1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani wawakilisha Syria Jumuiya ya Kiarabu

Admin.WagnerD26 Machi 2013

Viongozi wa upinzani wa Syria wamekalia kwa mara ya kwanza kiti cha uwakilishi wa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa hayo ulianza rasmi mjini Doha, nchini Qatar

https://p.dw.com/p/184F9
Heads of Arab states gather for a group photo during the opening of the Arab League summit in Doha March 26, 2013. A summit of Arab heads of state opened in the Qatari capital Doha on Tuesday expected to focus on the war in Syria as well as on the Israeli-Palestinian conflict. REUTERS/Ahmed Jadallah (QATAR - Tags: POLITICS ROYALS)
Viongizi wa mataifa ya kiarabuPicha: Reuters

Bendera ya wapinzani wa Syria imepeperushwa kwa mara ya kwanza, badala ya ile ya Syria, katika mkutano huo unaojumisha mataifa wanachama 22 ya kiarabu. Kitendo kinatajwa kuwa mwiba mwingine kwa utawala wa Assad pamoja na taarifa ya kundi hilo limemeguka meguka.

Mzizi wa pendekozo la kuruhusu uwakilisha wa upinzani katika kiti cha unachama ho ulitolewa mapema wiki hii na mawaziri wa mambo ya nje ya umoaja huo, katika mkutano wao wa awali wa maandalizi ya mkutano huu wa kilele wa viongozi wakuu.

The Syrian opposition flag is seen in front of the seat of the Syrian delegation at the opening the Arab League summit in Doha March 26, 2013. A summit of Arab heads of state opened in the Qatari capital Doha on Tuesday expected to focus on the war in Syria as well as on the Israeli-Palestinian conflict. REUTERS/Ahmed Jadallah (QATAR - Tags: POLITICS)
Bendera ya upinzani ya SyriaPicha: Reuters

Akifungua mkutano huo, Kiongozi wa Qatar, Sheikh Hamad bin Khalifa Al-Thani, aliomba wajumbe wa mkutano huo kuridhia wawakilishi upinzani, Ghassani Hitto na Ahmed Moaz al-Khatib  kukalia kiti cha Syria katika mkutano huo jambo ambalo lilikubaliwa na wajumbe wa mkutano.

Baraza la Usalama lisimamishe mapigano

Aidha katika hotuba yake kiongozi huyo wa Qatar amelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa, kusimamisha vitendo vya mauwaji vinavyoendelea nchini Syria na kuwafikisha katika mahakama ya kimataifa wale wote waliohusika na vitendio hivyo.

Kiongozi wa wa upinzani Moaz al-Khatib, mmoja kati ya wanaharakati maarufu sana katika vita dhidi ya rais Bashar al Assad amezungumza mbele ya viongozi wa mataifa hayo ya kiarabu. Jumapili iliyopita kiongozi huyo aliushtua upande wa upinzani pamoja na wanaomuunga mkoni kwa hatua yake ya kutangaza kujiuzulu kwa kuitupia lawama jumuiya ya kimataifa kushindwa kuwasaidia nchini Syria pamoja na watu kuendelea kuuwawa kila kukicha.

Pamoja na yote hayo yeye au mwenzake yeyote, miongoni mwa waliyopo katika mkutano huo wa kilele wa viongozi wa nchi za Kiarab, baada ya Jumuiya hiyo kusimamisha uanachama wa Syria 2011, kutokana na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji walikuwa wakipinga utawala wa Assad angeweza kuzungumza.

Mchango wa kuwasaidia Wapalestina

Katika hatua nyingine Qatar imetoa wito wa kufanyika kwa mchango wa haraka wa kiasi cha dola bilioni moja kuwasaidia Wapalestina katika Jerusalem ya Mashariki na ikatangaza kuchangia kuchangia kiasi cha dola milioni 250.

Hata hivyo Kiongozi wa Qatar akutoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo lakini mataifa ya kiarabu yana hofu kwamba ujenzi unaofanywa na Isreal katika eneo lililonje ya mipaka ya mwaka 1967 unafanya wazo la kuunda matifa mawili kati ya Israel na Palestina, lisitekelezeke.

Mwandishi: Sudi Mnette/rtr
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman