1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wananchi wa Algeria wapiga kura leo

17 Aprili 2014

Leo wananchi wa Algeria wamemiminika katika vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa rais ambao unasusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani.

https://p.dw.com/p/1Bk1X
Pichani ni rais wa sasa Abdel Aziz Bouteflika akigombea tena kiti cha urais
Pichani ni rais wa sasa Abdel Aziz Bouteflika akigombea tena kiti cha uraisPicha: Patrick Baz/AFP/Getty Images

Vituo vya kupiga kura vilifungulia tangu saa mbili asubuhi saa za Algeria kwa ajili ya zoezi hilo litakaloendelea kwa saa 11 zijazo. Wagombea wakuu katika uchaguzi huo ni rais wa sasa Abdel Aziz Boutefilika mwenye umri wa miaka 77 ambaye anagombea muhula wa nne licha ya afya yake kuwa mbaya na aliyekuwa waziri mkuu Ali Benflis mwenye umri wa miaka 69 ambaye anatajwa huenda akampa changamoto Bouteflika katika uchaguzi huu. Je wachambuzi wa mambo wanautazama vipi uchaguzi huu hasa ikizingatiwa mara zote nchini Algeria chaguzi zinakumbwa na utata na madai ya udanganyifu. Saumu Mwasimba amezungumza na Ahmed Rajab mchambuzi wa Kimataifa. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Josephat Charo