1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajali – Watu wanaoleta mabadiliko katika jamii

25 Juni 2012

Kwa kusikiliza kilio cha wakaazi wa mitaa ya mabanda, kuwaelimisha watoto yatima, juhudi za baadhi ya Waafrika zimesaidia sana kubadilisha hali ya mambo na kuufanya ulimwengu kuwa mahala bora pa kuishi.

https://p.dw.com/p/MAkc
Kulifanya bara la Afrika kuwa mahala pazuri zaidi kwa watoto kuishi - njia mojawapo ya kuleta mabadiliko kote AfrikaPicha: LAI F

David Kimaro ana umri wa miaka 26 na baba wa watoto 30. Hali hii si ya kawaida hasa ikizingatiwa umri wake. Hata hivyo watoto hawa hakuwazaa yeye. Ni watoto yatima ambao kwa mapenzi yake amejitikwa jukumu la kuwatunza na kuwalea. Wazazi wa Kimaro ndio walioanzisha mpango wa kuwapa makao baadhi ya watoto hawa yatima baada ya kuwapoteza wazazi wao. Na hapo David pia akafuata nyayo zao na kujitolea maishani kuwahudumia watoto hawa. Na ndipo akaanzisha makao ya watoto mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania na ambako sasa ni mkurugenzi wa makao hayo.

"Watu wanaoleta mabadiliko katika maisha ya wengine" ndio mada ya vipindi hivi vya redio vinavyokukutanisha na David na wengineo – Vijana waliojitolea maishani kuwasaidia wengine. Kwa mfano kuanzisha kituo cha redio ili kuwapa nafasi wakaazi wa mitaa ya mabanda kutoa sauti zao, kutundika mabango yenye ujumbe wa kupinga vita vya wenyewe kwa wenyewe au hata kuwa mwanariadha hodari ulimwenguni ili kuisaidia jamii yako.
Endapo unajiuliza nini unachoweza kufanya ili kuwasaidia wengine nchini mwako, Noa Bongo inakupa vidokezo na msukumo wa kufikia hilo!

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika lugha sita; Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharic. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani