1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani waongoza mapinduzi ya nne ya viwanda

Henrik Böhme9 Aprili 2014

Sekta ya viwanda ya Ujerumani inaongoza kwa teknolojia za uzalishaji wenye ufanisi. Lakini ikiwa inataka kuendelea hivyo, basi inahitaji kujiboresha zaidi, kwa mfano kwa mfano kwa kuungana na sekta ya teknolojia.

https://p.dw.com/p/1Bdgp
Mashine ya Robot ikiwa katika banda la kampuni ya Siemens.
Mashine ya Robot ikiwa katika banda la kampuni ya Siemens.Picha: DW/H. Böhme

Hii ndiyo mada kuu katika maonyesho ya Hanover, ambayo ndiyo makubwa zaidi ya sekta ya magari duniani. Muundo wa viwanda vya baadaye umekuwa ukionekana katika maonyesho ya Hanover kwa muda mrefu.

Hii imekuwa mada iliyojadiliwa kwa miaka kadhaa kila wakati wadau wa sekta hiyo wanapohudhuria maonyeshoya viwanda mjini Hanover. Ila mara hii mambo yanaonekana kuwa thabiti zaidi kiasi cha kuweza kushikika.

Kila mtu anazungumzia kiwanda 4.0, ambacho ni kiwango kilichoanzishwa na wajenzi wa mashine na viwanda wa Ujerumani miaka miwili iliyopita, na kinachotazamiwa kuwa mfano wa kuigwa duniani kote.

Mashine zitaanza kutumika kufanya kazi nyingi katika uzali´shaji w akiviwanda.
Mashine zitaanza kutumika kufanya kazi nyingi katika uzali´shaji w akiviwanda.Picha: picture-alliance/dpa

"Kipya hapa ni kwamba sisi tunaanza kufikiria kwa mtazamo wa wateja. Laazima tuanze kutumia kiwanda 4.0 ili kuifanya mifumo yetu iwavutie wateja. Makampuni makubwa ya programu yako nchini Marekani, na huko pia kuna hatari zake, Lakini mimi binafsi sina hofu, kwa sababu sisi tunahakikisha kuwa katika uhandisi wa kiufundi tunaendelea kuongoza," anasema Reinhold Festge, mwenyekiti wa chama cha wajenzi wa mashine na viwanda VDMA.

Msukumo mpya unahitajika, kwa sababu biashara muhimu za Ujerumani hazijafanya vizuri sana katika miaka ya hivi karibuni. Na msukumo huu utaletwa kwa kuunganisha uzalishaji na ulimwengu wa teknolojia mpya ya mawasiliano.

Hilo halitokei lenyewe, na hivyo mtu anaweza kuelewa matamshi ya onyo kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda cha Ujerumani BDI, Ulrich Grillo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo - kwamba Ujerumani inaweza kupoteza uwiano.

"Nilimaanisha kile hasa tunachokiona hapa. Tuko katika soko la ulimwnegu wa mawasiliano ya habari na teknolojia, ambako sisi Ulaya tuko nyuma na Wamarekani wanaongoza. Lakini tunatumia teknolojia hizi ili kuipeleka mbele sekta kwa kutumia mitambo inayojiendesha yenyewe, na teknolojia ya udhibiti.

Huko tuna uhakika zaidi, na mtu anaweza kusema sisi ndiyo tunaongoza katika nyanja hiyo. Hiyo inamaanisha kwamba tunapaswa kushirkiana, tunahitaji kujenga mitandao mipya katika sekta yetu, na hilo ndiyo linapaswa kuwa lengo."

Hiyo ni changamoto kubwa kwa makampuni imara ya kati ya Ujerumani yanayojenga machine na viwanda. Moja ya makampuni hayo ni ile inayoogoza kwa bidhaa zake, ya Weidmüller kutoka jimbo la North Rhine-Westphalia. Nyaya zake na viunganisho vinavyouzwa duniani kote vinahakikisha kuwa mashine zinaweza kuwasiliana.

Banda la teknolojia la Uholanzi
Banda la teknolojia la UholanziPicha: picture-alliance/dpa

"Hapo tutakuwa katika hatari ya kupoteza uwiano - ambapo uwiano ndiyo neno lisilo sahihi, lakini kupoteza uongozi wetu tuliokuwa nao kwa karibu miaka miwili. Tunapaswa kuutetea uongozi huu kupitia utafiti, ushirikiano na vyuo vikuu, taasisi na vyama ili kuendelea kuongoza duniani hata kwa Kiwanda 4.0," alisema Peter Köhler, Mkrugenzi wa bodi ya kiwanda hicho.

Washindani watayasikia hayo kwa shauku na hawatakuwa tayari kuwaachia Wajerumani waendelee kunufaika bila ushindani. Na kuna mengi ya kufanya kufanikisha dhana ya kiwanda cha baadaye.

Kama alivyosema meneja mwandamizi mbele ya Kansela Angela Merkel alipotembelea banda ya kampuni ya Siemens siku ya Jumatatu, badala ya teknolojia ya viwanda 4.0, kilichopo sasa ni teknolojia ya 3.8. Ni bado kuamua hasa ni nani atakaeongoza mapinduzi ya nne ya sekta ya viwanda.

Mwandishi: Böhme Henrik
Tafsiri: Iddi Ssessanga
Mhariri: Josephat Charo