1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafusi wa Mursi wajiimarisha Misri

Admin.WagnerD12 Agosti 2013

Wafuasi wa Kiongozi wa Misri aliyeondolewa madarakani, wamejiimarisha katika maeneo ya kambi baada ya jeshi la polisi nchini humo kusema watazizingira kambi zao na kuwatawanya katika kipindi kisichozidi masaa 24.

https://p.dw.com/p/19NyJ
epa03820702 Supporters of the Muslim Brotherhood attend a protest in support of ousted Egyptian President Mohamed Morsi outside the Rabaa al-Adawiya mosque, in Cairo, Egypt, 11 August 2013. Morsi and Muslim Brotherhood supporters intend to hold more rallies calling for a reinstatement of ousted President Morsi. Egypt's interim government insisted they will disband the protest camps after Eid al-Fitr, the Muslim holiday marking the end of Ramadan the same day. EPA/KHALED ELFIQI
Waandamaji MisriPicha: picture-alliance/dpa

Kitisho cha jeshi la polisi cha kuvunja mikusanyiko miwili ya wafuasi wa Chama cha Udugu wa Kiislamu, inafanya kuwepo kwa mashaka ya uwezekano wa kuzuka tena vurugu nchini Misri. Jeshi la taifa hilo mwezi uliopita lilimuondoa madarakani rais Mursi baada ya maandamano ya mamilioni ya watu kuupinga utawala wake.

Hatua ya sasa ya polisi, inaelezwa kuwa jeshi hilo linaweka milango wazi kabisa ya kutokea vurugu za makabiliano kati ya jeshi lenye kuungwa mkono na serikali na maelfu ya wafuasi wa rais alieondolewa madarakani, Mohammed Mursi.

Kauli ya waandamanaji

Waandamanaji tayari wamekwisha sema hawawezi kuondoka katika viwanja hivyo mpaka rais huyo aliendolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi Julai 3 mwaka huu arejeshwe madarakani.

Supporters of Egypt's ousted President Mohammed Morsi shout slogans under his posters following Friday prayers in Nahda square, where protesters installed their camp near Cairo University in Giza, southwest of Cairo, Egypt, Friday, Aug. 9, 2013. Protesters demand Morsi's reinstatement, restoration of the suspended constitution drafted under Morsi and the return of his Islamist-dominated legislative council which was also disbanded. The Arabic on the posters reads, "No for coup." (AP Photo/Amr Nabil)
Wafuasi wa rais Morsi katika uwanja wa Giza mjini CairoPicha: picture-alliance/AP Photo

Jitihada za mataifa ya magharibi kuumaliza mgogoro huo zimeshindwa. Mwisho wa juma, polisi imesema itadhibiti mkusanyiko wao wowote kwa kutumia maji ya kuwasha katika kuwasambaratisha. Lakini wanaharakati wa haki za binaadamu wameonya kwamba kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji kutasababisha vitendo vya umwagikaji damu.

Kadhia ya maandamano ya Misri

Uongozi mpya wa Misri umesema maandamano hayo yanawatoa hofu raia wengine wa Misri, kusababisha vurugu zinazopelekea mauwaji na na kusababisha msongamano wa magari.

Viongozi katika mikusanyiko hio wamesema wametekeleza jukumu hilo kwa amani na wamevilalamikia vyombo vya usalama kwa kusababisha machafuko. Zaidi ya watu 250 wameuwawa tangu kuondolewa madarakani kwa Morsi.

Katika mkusanyiko mkubwa wa wafuasi hao mjini Cairo wachuuzi wa bidhaa ndogondogo wamesema wameuza idadi kubwa ya vifaa vya kujikinga na mashambulizi ya polisi kama vya kuziuia athari za mabomu ya machozi na vinginevyo. Wameweka vizuizi vilivyojengwa kwa saruji pamoja na mbao kwa ajili ya kuzuia magari lenye silaha ya vyombo vya usalama kuingia katika eneo hilo.

Kwa upande wao maafisa wa usalama wamesema wataweka vizuizi vya kuingia katika maeneo hayo ya maandamano kwa lengo la kuzuia yeyote kuingia, na kwamba mmoja kati ya maafisa hao alisema hatua hiyo ingalianza tu baada ya jua kuchomoza leo hii.

Lakini hata hivyo mpaka mapema asubuhi ya leo hakukuwa na ishara yoyote ya vikosi kuwasili katika maeneo hayo na kwamba serikali haijasema muda gani hasa itakwenda katika maeneo hayo ya waandamanaji.

Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhariri:Yusuf Saumu