1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wa Afrika wachunguzwa kuhusu Ebola

21 Novemba 2014

Wachezaji kutoka bara la bara Afrika wanachunguzwa kwa kina na vilabu vya Bundesliga wanapotoka kutumikia nchi zao kwa ya hofu ya ugonjwa hatari wa Ebola.

https://p.dw.com/p/1DrE7
Bildergalerie Afrikanische Fußballspieler Pierre-Emerick Aubameyang
Pierre Emerik Aubamiyang kutoka GabonPicha: Getty Images/S. Steinbach/Bongarts

Wachezaji wa bara la Afrika wanaorejea kutoka katika michezo ya kimataifa na timu zao za taifa wanafanyiwa uchunguzi wa kina na vilabu vyao katika Bundesliga kutokana na wasi wasi juu ya ugonjwa wa Ebola, lakini timu hizo hajaingia katika taharuki na zinafahamu zinalazimika kuwaruhusu wachezaji walioteuliwa kuchezea timu zao kwa ajili ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani kuanzia Januari.

Fußball Bundesliga 11. Spieltag TSG 1899 Hoffenheim - 1. FC Köln
Mchezaji Anthony Ujah wa FC Kolon kutoka NigeriaPicha: picture-alliance/dpa

Madaktari wa timu wanafanya uchunguzi wa kina kwa wachezaji hao ambao hawaruhusiwi kuanza mazowezi na timu zao za vilabu hadi baada ya uchunguzi.

Morocco ilivuliwa jukumu hilo baada ya ombi lao la kuahirishwa kwa fainali hizo kukataliwa wakidai kuwa na wasi wasi kuhusu kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

Shirika la afya ulimwenguni halikupinga kufanyika fainali hizo nchini Morocco.

Ligi za Ulaya zaanza tena

Na katika bara la Ulaya , timu zinarejea dimbani kwa mara nyingine tena wiki hii, baada ya kusita kwa ligi kwa muda wa wiki mbili kutokana na michezo ya kimataifa , barani Ulaya kuwania kufuzu katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya , Euro 2016 nchini Ufaransa , fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani , pamoja na michezo mbali mbali ya kirafiki. Nchini Uhispania Real Madrid ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchi hiyo La Liga inateremka dimbani leo jioni kupambana na Eibar kutoka jimbo la Basque.

FC Barcelona vs. Real Madrid 25.10.2014
Cristiano Ronaldo wa Real MadridPicha: AFP/Getty Images

Tofauti na uwanja maarufu na mkubwa wa Real , Santiago Bernabeu ambao unauwezo wa kusheheni mashabiki 85,000 , uwanja wa Eibar una nafasi 5,000 tu za mashabiki, na imelazimu kujenga viti vya muda kuweza kuwapatia nafasi mashabiki kumuangalia Cristiano Ronaldo na wenzake wakisakata kabumbu jioni ya leo.

Licha ya unyonge wa Eibar lakini iko katikati mwa msimamo wa ligi hiyo. Barcelona ni wenyeji wa Sevilla , ambao wako pointi mbili tu nyuma ya Barca. Michezo mingine ni pamoja na Atletico Madrid ikipambana na Malaga, Deportivo La Coruna inaikaribisha Real Sociedad. Jumapili ni zamu ya Rayo Vallecano ikipimana nguvu na Celta Vigo, Levante ina miadi na Valencia , Elche na Cordoba na Villarreal inatiana kifuani na Getafe.

Nchini Italia , pambano la kwanza la watani wa jadi mjini Milan msimu huu linampa kocha Roberto Mancini mtihani wake wa kwanza wakati akirejea katika kiti cha kibarua cha Inter Milan , wakati Lazio Rome inakuwa mwenyeji wa mabingwa na viongozi wa ligi ya Italia Serie A Juventus Turin ikiwania ushindi ambao unaweza kusaidia timu hasimu ya Roma.

Mapambano mengine ni pamoja na Napoli ikipambana na Cagliari, Parma na Empoli, na Udinise iko nyumbani ikiisubiri Chievo Verona.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Khelef