1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utandawazi - Rafiki na adui wa Afrika

25 Mei 2011

Vipindi vya Noa Bongo vinachunguza kwa kina athari za utandawazi barani Afrika. Kupitia vipindi vyetu wasikilizaji wanaweza kukutana na watu wanaochangia kuufanikisha utandawazi na wale wanaoathiriwa na utandawazi.

https://p.dw.com/p/RPwl
Baadhi ya wataalamu wanaamini utandawazi utasaidia kuimarisha uchumi wa AfrikaPicha: Corbis

Vipindi vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako vinaonyesha jinsi utandawazi unavyowanyanyua watu kutokana na umaskini na vipi wengine wanavyotumbukia zaidi katika umaskini uliokithiri kutokana na utandawazi.

Wakati wakosoaji wa utandawazi walipokutana mjini Nairobi, Kenya mnamo mwaka 2007 kwenye Jukwaa la Kimataifa la Kijamii, walikubaliana juu ya ujumbe ulio wazi kabisa: Utandawazi ni mojawapo ya sababu kubwa za maendeleo duni na umasikini barani Afrika. Hata hivyo serikali za mataifa ya magharibi na mashirika ya fedha ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, yanasisitiza kwamba Afrika lazima ifungue masoko yake na iongeze biashara na ulimwengu wa magharibi ili iweze kukua kiuchumi.

Sura mbalimbali

Vipindi vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako havijiingizi katika vita hivyo. Badala yake huchambua sura mbalimbali za utandawazi barani Afrika. Waandishi wetu wanazungumza na watu walioyaacha makazi yao kwenda kutafuta maisha mazuri katika miji mikuu ya nchi za Afrika na hata barani Ulaya. Wanawatambulisha wafanyabiashara wa Afrika wanaonufaika kutokana mfumo wa uchumi wa utandawazi na wanaangalia jinsi kilimo, uti wa mgongo wa uchumi wa Afrika, kinavyobadilika kutokana na athari za utandawazi.

Vipindi vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic. Mradi huu unafadhiliwa na wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani.

Hisia za wasikilizaji

Soma maoni ya watu wengine jinsi wanavyofikiri juu ya mfululizo wa vpindi vyetu kuhusu "Utandawazi - Rafiki na adui wa Afrika" katika ukurasa ufuatao.