1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usafi na Afya - Jinsi ya kujikinga na maambukizi

2 Agosti 2010

Ugonjwa wa Kuhara husababisha vifo vingi barani Afrika na hutokea aghalabu. Hata hivyo ni wachache tu wanaozifahamu njia mujarab za kuzuwia maambukizi yanayosababishwa na uchafu.

https://p.dw.com/p/OaDz
Kuosha mikono ni njia moja muhimu ya kujikinga na maambukiziPicha: LAIF

Ungana mashujaa wetu chipukizi walio katika harakati za kupambana na ugonjwa huu hatari. Mbali magonjwa ya Malaria na HIV na Ukimwi, yapo mengi mengine yanayosababisha vifo barani Afrika.Watoto wadogo ndio walio katika hatari zaidi ya kufariki wanapoambukizwa ugonjwa wa Kuhara.Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, Ugonjwa kuhara husababisha vifo vya watu milioni 2.2 kila mwaka. Wengi wao huathirika kwasababu ya kutumia maji yasiyo salama kwa kunywa,kupikia na kufua pamoja na kuosha vyombo. Jee, Ugonjwa huo unapaswa kuendelea kusababisha maafa barani Afrika?

Kijana mdogo Sam na familia yake wanajitahidi sana kupambana na mkazi huyo aliyewavamia. Sam na mdogo wake Fatu wako taabani na afya yao inazidi kudhoofika, tena kwa haraka. Jee watapona? Jirani yao Maria, anayejifanya kujua yote, kamwe hakosi ushauri na mapendekezo ya usaidizi. Kutokana na yote hayo, Chemu, rafikiye Sam, ameamua kutumia mbinu zake mwenyewe kupambana na ugonjwa huo.

Katika makala haya ya Noa Bongo: Jenga maisha yako, sikiliza jinsi Sam, familia yake na marafiki wanavyotatizwa na ugonjwa wa Kuhara vilevile utajifunza chanzo,njia kujikinga pmaoja na tiba yake.

Michezo ya Noa Bongo: Jenga Maisha yako inaweza kusikilizwa katika lugha sita tofauti: Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kihabeshi. Mradi huu unaungwa mkono na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani