1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhifadhi wa misitu kwa maisha bora Kenya

2 Septemba 2014

Muongo mmoja uliopita mkoa wa Kasigau ulipo kusini mashariki mwa Kenya ulikuwa jangwa kwa ukataji miti ovyo.Lakini hivi sasa hali imebadiliko ambapo mkoa huo umukuwa chanzo cha wengi kujipatia fedha kwa rasilimali.

https://p.dw.com/p/1D5Mc
Kenia Waldbrand Waldbrände Feuer 2012
Uharibufu wa mazingira nchini KenyaPicha: AP

Mmoja kati ya waakazi wa kwanza wa eneo hilo Mercy Ngaruiya ambaye pia ni kiongozi wa jamii hiyo aliliambia shirika la habari la IPS kuwa hali halisi ya mkoa huo ilikuwa jangwa ,hakukuwa na miti katika eneo lake wakati anahamia ,eneo lote lilikuwa kavu watu walikuwa wakikata miti na kuchoma misitu kwa ajili ya kijipatia kuni na kuendesha maisha yao

Anaongeza kuwa umasikini na ukosefu wa ajira ndio chanzo cha hayo yote pia jamii ilikuwa na huduma duni za afya, maji safi, na Elimu

Vitendo vya ukataji miti ovyo

Rais wa idara ya wanyamapori, ujenzi na kampeni ya ukataji miti na uharibifu wa mazingira(REDD) Mike Korchinsky aliiambi pia IPS kuwa anakumbuka alipofika eneo hilo pia aliweza kusikia sauti za shoka na watu wakikata,kukata miti ovyo ni hatari kwa sababu inatoa uchafu wa haraka unaotokana na hewa ya kabon ambayo imekuwa ikihifadhiwa na misitu kwa karne nyingi sasa ilazimika kuifadhiwa na anga hivyo hakuna ulazima wa kutenga carbon kwa kuwa inazalishwa na shughuli za binadamu

Insel Lamu Kenia
Mandhari ya kisiwa cha LamuPicha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Wilaya mbili zilowekwa kwa ajili ya majaribio ya kukabiliana na suala la ukataji miti ya idara ya wanyamapori, ujenzi na kampeni ya kuzuia ukataji miti na uharibifu wa mazingira [REDD+] ni wilaya za Tsavo mashariki na Tsavo magharibi zilizo kilomita 150 kutoka kaskazini magharibi mwa mwambao wa mombasa .Mradi huo umeanza kuleta mabadiliko polepole ya kiuchumi baada ya kuanzishwa mkoani Kasigau sasa umeweza kutoa elimu kwa wakazi 100,000

Ufumbuzi wa kupunguza umasikini

Mradi huo wa Kasigau ni wa kwanza kuthibitishwa nchini Kenya ambapo jamii sasa inaishi katika eneo hilo na kujipatia fedha kwa kuhifadhi rasilimali za asili.

Msimamizi wa eneo la Kasigau Pascal Kizaka Aliiambia IPS kuwa mradi wa REDD + umekuwa na ufumbuzi wa kweli na moja kwa moja kwa kupunguza umaskini.

Kizaka anasisita kuwa Mbali na uhifadhi, umekuwa sehemu ya faida inayowezesha ujenzi wa madarasa 20 ya kisasa katika shule za mitaa, misaada ya kifedha kwa zaidi ya wanafunzi 1,800 , na ujenzi wa kituo cha afya na sekta ya kuboresha viwango vya maisha,

Ngaruiya anaongeza kuwa mambo sasa yamebadilika hasa tangu wanakijiji wenzake walipokubaliana kuhifadhi mazingira na wanaendelea kuboresha

Naye mkazi mmoja wa eneo hilo Nicoleta Mwende aliiambia IPS kuwa kwa sasa hawana haja tena ya kukata miti kwa ajili ya mkaa,sasa wanatumia gas asilia na mkaa uliotokana na magome ya mti, wanaendelea kupika na kutunza mazingira


Mafanikio hayo mapya ya ukanda huo yanayotokana na mradi wa REDD+ ni kuwawezesha maelfu wa wakazi kuachana na uharibifu wa misitu na kukabiliana na maisha mpya endelevu, hata hivyo kwa sasa mradi huo unazalisha zaidi ya dola milioni moja kwa mwaka kutokana na mauzo ya kabon kwa dola nane kwa tani juu ya ubadilishaji wa Kabon Africa


Lakini kulingana na Alfred Gichu mtaalamu wa misitu anasema mabadiliko ya hali ya hewa katika misitu,inaweza kutuzwa iwapo shirika la serikali litamua kuhifadhi misitu hadi hapo baadaye itakapo toa mikopo ya biashara ya kabon


Ripoti ya mafanikio 2013 inatoa mfano wa mradi wa Kasigau REDD +, kutoka mwaka 2012 mapato yaliyotokana na uuzaji wa mikopo kwa hiari ilifikia dola milioni 1.2. Kwa mujibu wa UNEP 2013 Uzalishaji uendelea kwa kupanda miti katika mashamba, shule na taasisi nyingine za umma; kuzuia uvunaji wa miti katika misitu ya umma; na uhamasishaji na serikali na watu binafsi kuunga mkono juhudi za kisera nchini Kenya kutunza misitu

Mwanamazingira John Maina anasema serikali,sekta zisizo za kiraina na mashirika yasiyo ya kiserikali wanao wajibu wa kufanya kazi pamoja na kuimarisha kanuni, pamoja na kusimamia wakenya katika mradi huo wa kaboni na jinsi gani waweze kujipatia fedha

Mwandishi:Nyamiti Kayora/IPS
Mhariri:Yusuf Saumu