1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwalimu wa udereva kutoka Ghana afundisha watu Berlin

2 Agosti 2016

Kuendesha gari katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari Berlin si kazi rahisi kwa baadhi ya watu. Victor Boadum kutoka Ghana ni miongoni mwa Waafrika wachache wanaotoa mafunzo ya kuendesha magari.

https://p.dw.com/p/1JaHR
Mwalimu wa udereva kutoka Ghana afundisha watu Berlin
Mwalimu wa udereva kutoka Ghana afundisha watu BerlinPicha: DW/D. Pelz

Mwalimu wa udereva kutoka Ghana afundisha watu Berlin

"Ni jambo la kipekee kuwafundisha wanafunzi kutoka Afrika, najua mie ni mmoja wao, najua uwezo wao wa akili, najiona kama nimevaa viatu vyao, najisikia fahari kuwa pamoja nao na kuwafanikisha kumudu kuendesha magari," anasema mkufunzi huyo.

Kwa upande wake mwalimu Victor Boadum anaifahamu vema mitaa ya jiji la Berlin kwani amekuwa akiishi katika jiji hilo tangu mwaka 1979. Baada ya kufanya kazi katika ubalozi mmoja wa nje na kwa miaka kadhaa akijiajiri mwenyewe, baadaye aliamua kubadilisha fani.
Victor Boadum anapata wateja wengi kutoka Afrika
Victor Boadum anapata wateja wengi kutoka AfrikaPicha: DW/D. Pelz
Anasema baadhi ya watu hawakudhani kuwa ni mwalimu wa kufundisha watu kuendesha magari ana wamekuwa wakimuuliza kama yeye ndiye anaosha magari na baadhi yao nyakati zilizopita walithubutu kusimamisha magari yao na kumuuliza kama yeye hufanya kazi hiyo ya kuwaelekeza watu jinsi ya kuendesha magari. Anasema watu hao wamekuwa wakionyesha kufurahia kazi yake hiyo kwani hawajawahi kumuona mtu raia wa Afrika akifanya kazi hiyo.
Azifahamu changamoto
Somo la leo ni jinsi ya kugeuza gari wakati unapokuwa unaendesha usisahau kuangalia vioo vya nje vya kuongozea gari " anasema Victor Boadum wakati anapomuelekeza mwanafunzi wake Sharon wakati waliposimama katika taa za barabarani za kuruhusu kupita au kusimamisha magari.
Victor Boadum akiwa na mmoja wa wanafunzi wake wa udereva
Victor Boadum akiwa na mmoja wa wanafunzi wake wa uderevaPicha: DW/D. Pelz
"Wakati nilipokutana na mwalimu Victor nilifurahi sana , kwa sababu sikuwahi kumuona mwalimu mwenye asili ya Afrika anayewafundisha watu jinsi ya kuendesha magari hapo kabla nchini Ujerumani na alionekana kuwa mvumilivu kwangu nami nikaamua kuwa ndiye atakuwa mwalimu wangu katika kuniwezesha kujua kuendesha gari " anasema mwanafunzi huyo Sharon Uzo ambaye pia ni mwanafunzi wa fani ya tekinolojia ya habari na mawasiliano.
Mwalimu Victor Boadum alisikika pia akimueleza mwanafunzi wake kukumbuka kuwa matumizi ya taa nyekundu barabarani yanafanana awapo jijini Free Town, Accra, New York na hata jijini Berlin na kuwa anapofanya mitihani yake ya kufuzu hawezi kumjibu msimamizi wa mtihani kuwa barani Afrika taa nyekundu inamaanisha kuwa ni kijani.
Victor Boadum huchukua muda wa kutosha kuwaelezea wanafunzi wake sheria za barabarani
Victor Boadum huchukua muda wa kutosha kuwaelezea wanafunzi wake sheria za barabaraniPicha: DW/D. Pelz
Anasema kufundisha watu jinsi ya kuendesha magari ni kazi nyingine na kusikiliza pia ni kazi nyingine. Anaongeza kuwa kuwafundisha waafrika jinsi ya kuendesha magari kunatoa nafasi pia ya kusikia mengi kutoka kwao jinsi wanavyojitahidi kuufahamau mfumo wa maisha nchini Ujerumani na pia wakati mwingine urasimu nchini humo.
Mwalimu Victor anasema anapomaliza kazi ya ukufunzi wa magari katika siku badaye hufanya majukumu mengine kwani yeye ni kiongozi wa kundi la watu zaidi ya 40,000 katika mkoa wa Ashanti nchini Ghana jukumu ambalo anaona ni heshima kubwa kwake ingawa anasema amekuwa akipata wakati mgumu kutekeleza majukumu yake na wakati mwingine amekuwa akitumia simu na barua pepe katika kutekeleza kazi zake kama kiongozi wa kundi hilo.