1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirikisho la Soka Nigeria lamtimua rais wake

25 Julai 2014

Shirikisho la Soka la Nigeria – NFF limemtimua rais wake Aminu Maigari. Hivi karibuni iliingilia kati mgogoro huo na kuipiga marufuku kwa muda Nigeria dhidi ya kushiriki katika soka la kimataifa

https://p.dw.com/p/1Cj3P
Nigeria Fußball Logo Nigeria Football Federation NFF
Picha: Franck Fife/AFP/Getty Images

Maigari anatuhumiwa kwa “usiri unaozunguka matumizi yote ya kifedha katika shirikisho hilo” na kushindwa kuitisha kikao cha kamati kuu kwa kipindi cha miezi minane iliyopita. Kamati kuu ya NFF ilipitisha kura ya kutokuwa na imani na rais wake, na ikaidhinisha kutimuliwa kwake maramoja kwa misingi ya matumizi mabaya ya fedha, na uongozi mbaya. Mike Okeke Umeh alichaguliwa kuwa kaimu rais, kabla ya kuandaliwa uchaguzi mpya mnamo Agosti 26.

Mapema mwezi huu, Nigeria ilipigwa marufuku kwa muda na FIFA kwa sababu kuwa serikali inaingilia kati masuala ya shirikisho la soka la taifa. Mahakama kuu iliamuru kuvunjwa kwa ofisi kuu ya NFF, siku moja tu baada ya Super Eagles kuondolewa nje ya Kombe la Dunia na Ufaransa katika awamu ya 16 za mwisho.

Mahakama pia ilimpa jukumu Waziri wa michezo kumchagua kaimu kiongozi, ambaye aliitisha uchaguzi mpya. FIFA iliipiga marufuku nchi hiyo na ikabatilisha uamuzi wake siku tisa baadaye wakati Maigari aliporejeshwa uongozini kufuatia amri ya mahakama.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef