1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la bomu jijini Nairobi

24 Aprili 2014

Watu wanne waliuawa katika mripuko wa gari uliotokea jana jioni kwenye kituo cha polisi cha Pangani mjini Nairobi, Kenya, miongoni mwa wahanga wakiwemo maafisi wawili wa polisi.

https://p.dw.com/p/1BnmH
Bomu limeripuka kwenye eneo la Eastleigh mjini Nairobi
Bomu limeripuka kwenye eneo la Eastleigh mjini NairobiPicha: Reuters

Kisa hicho kilifuatia hatua ya polisi kuwakamata washukiwa wawili kwenye taa za barabarani, na kuwapeleka kituoni ili kuhojiwa. Mahali ulipotokea mripuko huo si mbali na mtaa wa Eastleigh wenye wakazi wengi wa asili ya kisomali, ambao miongoni mwao wanatuhumiwa kuliunga mkono kundi la Al-Shabab la nchini Somalia. Mtaa huo umekuwa ukishuhudia msururu wa mashambulizi mnamo siku za hivi karibuni, na swali linaloibuka ni kwanini kama wakazi wa mtaa huo wanahusika na mashambulizi hayo, Kwa nini yafanyike mahali jamii yao inakoishi! Daniel Gakuba amemuuliza mtafiti wa Taasisi ya Kimataifa ya mafunzo ya Usalama, ISS, jijini Nairobi, Emmanuel Kisiangani.

Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri: Josephat Charo