1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari ya Uganda dhidi ya Ukwimi

11 Desemba 2014

Moja kati ya mataifa ya Afrika yaliyoathiriwa vibaya na Ukimwi, Uganda imeweza kupunguza viwango vya maambukizi ya maradhi hayo kwa kugawa dawa za bure na mipira ya kinga kwa wanaume.

https://p.dw.com/p/1E1sd
Krankenhäuser restlos überfordert
Picha: DW/S. Schlindwein

Mbali na hilo pia imeanzisha kampeni ya kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi -HIV.

Pamoja na jitihada hizo lakini bado utoaji wa tiba madhubuti katika kukabiliana na janga hilo bado upo katika mashaka.

Muuguzi Margreth Nanyonga ambae yupo katika mpango wa kuhudumia wanaoishi na virus vya Ukimwi anazungumzia ugumu wa kupatikana dawa za kurefusha maisha katika kituo cha afya cha Uganda.

Muuguzi huyo anasema kiasi ya watu 900 kati ya jumla ya watu 2000 kwa kawaida wanaohudumiwa katika kituo hicho kilichopo mji wa Kyetume, mashariki mwa Kampala wanaishi na virusi vya Ukimwi.

Anasema miaka miwili iliyopita walikuwa 600. Na kwamba idadi ya watu wanaojiandisha kwa ajili ya dawa za kurefusha Maisha inazidi kuongezeka. Ameongeza kusema kwa hivi sasa kituo kimekuwa kimbilio la watu kufuata dawa.

Aids Medikamente werden in Uganda kostenlos verteilt
Mgonjwa akipatiwa dawa nchini UgandaPicha: DW/S. Schlindwein

Lakini kuwepo kwa wagonjwa zaidi wa Ukimwi katika taifa hilo ambalo ni miongini mwa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo barani Afrika ambapo baadhi ya viijjiji nusura viangamizwe na janga hilo katika miaka ya tisini hakumaanishi nchi hiyo imeshindwa kukabiliana nao.Ukweli wa mambo ni kinyume na dhana hiyo.

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini Uganda yamepungua kwa asilimia 7.3 ya idadi ya watu kwa mwaka 2011 kutoka asilimia 18.5 mwaka 1992, na hii ni kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mashirika ya UNAIDS na UNICEF inasema idadi ya maambukizi mapya kwa mwaka huu inakadiliwa kupungua na kufikia watu 137,000 kutoka juu ya watu 162,000 mwaka 2011.

Mkurugenzi wa shirika la UNAIDS Mussa Bungudu anasema Zaidi ya asilimia 90 ya wanawake wajawazito nchini Uganda walio na virusi vya Ukimwi wapo katika matibabu na hii inasaidia kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa wameathiika.

Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: picture alliance/empics

Watu kama Richard Aliwaali, ambaye amekuwa akiishi na virusi vya Ukimwi tangu mwaka 1998, ameungana na wafanyakazi wa afya kuhamasisha jamii kukabiliana na VVU. "Tunawambia watu wasiogope,tunawambia watu tuna virusi vya ukimwi na hivyo hawatakiwi kuwanyoshea vidole watu walioathirika",alisema mzee mwenye miaka 49 ambaye mke wake alifariki mwaka 2013.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka mwaka 1986 Rais Yoweri Museveni pia alianzisha kampeni ya kuhamasisha vijana kutofanya mapenzi kabla ya ndoa,kuwa na ndoa ya mke mmoja na kutumia kondomu kama hawawezi kujizuia.

Naibu waziri wa afya Sarah Opendi alisema idadi ya kondomu zinazogawiwa na serikali imeongezeka na kufikia milioni 100 mwaka huu kutoka milioni 85 mwaka 2012.

Aliongeza kuwa mahitaji ni makubwa lakini kutokana na matatizo ya kifedha wana uwezo wa kununua robo ambayo ya kile kinachoitajika,hii inaonyesha kweli watu wanatumia kondomu.

Lakini kampeni ya Rais Museveni kuwataka Waganda kuwa na mke mmoja imekuwa ya mafanikio madogo.

Mwandishi:Nyamiti Kayora/DPE

Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman