1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rudisha: tusitumie dawa za kuongeza nguvu

15 Desemba 2014

Bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 800 Mkenya David Rudisha amewaonya wanariadha wenzake kuwa wanakabiliwa na kitisho cha kuichafua sifa ya taifa hilo kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.

https://p.dw.com/p/1E4Mb
London 2012 - Leichtathletik
Picha: picture-alliance/dpa

Kenya, ambayo kitamaduni, ambayo wanariadha wake wa vipaji vya mbio za masafa marefu ni chanzo cha fahari ya kitaifa, ilishangazwa na ufichuzi kuwa Rota Jeptoo, mwanariadha bora mwanamke ulimwenguni kwa sasa katika mbio za marathon, aligundulika kutumia dawa zilizopigwa marufuku.

Rudisha anasema kenya inafahamika kwa sifa yake nzuri katika riadha, na imekuwa ikijivunia wanariadha wanaofany avyema katika jukwaa la kimataifa bila kujihusisha na dawa za kuongeza nguvu mwilini. Anaongeza kuwa wanaraidha wanahimizwa kutia bidii ili kupata mafanikio kutokana na vipaji vyao, na wala siyo kutumia njia za mkato. Kwa sababu kufany ahivyo unaharabu siyo tu sifa ya kenya bali pia ya mchezo.

Rudisha aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika “Olimpiki ya WaMasaai”, ambayo ni siku ya michezo iliyoandaliwa na watunzi wa mazingira ikiwa na lengo la kutoa njia mbadala ya kuonyesha nguvu za mashujaa wa Kimasaai, ambao kwa vizazi vingi wanadhihirisha ukomavu wao kwa kumuua simba. Rudisha mwenyewe ni Mmasaai, ndiye msimamizi wa michezo hiyo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu