1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pistorius: Hana hatia ya kuuwa kwa kukusudia

11 Septemba 2014

Jaji katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha wa Afrika kusini anayekimbilia miguu ya bandia Oscar Pistorius,Thokozile Masipa ameonekana kuelekea kutoa hukumu dhidi ya mwanariadha huyo kwa kosa la uzembe wa kuuwa.

https://p.dw.com/p/1DAd7
Südafrika Mordprozess Oscar Pistorius Gericht in Pretoria 11.09.2014
Oscar Pistorius akiwa mahakamani mjini PretoriaPicha: Reuters/P. Magakoe

Jaji Thokozile Masipa alimwondolea Oscar Pistorius makosa ya kuuwa kwa kukusudia na mauaji, katika kesi ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Jaji Thokozile Masipa amesema waendesha mashtaka hawajathibitisha bila shaka yoyote kwamba Pistorius mwenye umri wa miaka 27 , ana hatia ya kuuwa kwa kukusudia.

Südafrika Mordprozess Oscar Pistorius Gericht in Pretoria 11.09.2014
Jaji Thokozile Masipa akisoma majumuisho ya kesi dhidi ya PistoriusPicha: picture-alliance/K. Ludbrook

"Uzembe wa kuuwa unaostahili kuadhibiwa ndio hukumu sahihi," amesema jaji huyo, lakini hakutoa hukumu rasmi katika kesi hiyo ya kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake mwenye umri wa miaka 29 kabla ya kuiahirisha kesi hiyo kwa mapumziko ya chakula cha mchana leo.

Bado Pistorius atakwenda jela?

Uzembe wa kuuwa unaostahili kuadhibiwa , una maana ya uzembe wa mauaji. Iwapo Pistorius ataondolewa kosa la mauaji , bado atakwenda jela kwa miaka kadhaa iwapo ataonekana kuwa alichukua hatua ya kizembe katika kifo cha Steenkamp.

Pistorius amekiri kufyatua risasi mara nne ambazo zimesababisha kifo cha mpenzi wake Steenkamp katika siku ya wapendanao mwaka jana.

Oscar Pistorius Urteilsverlesung 11.09.2014
Oscar Pistorius kizimbaniPicha: Reuters/P. Magakoe

Pistorius anasema alidhania kuwa ni mtu aliyeingia katika nyumba yake kwa azma ya kufanya uhalifu na amemuua kwa bahati mbaya.

Upande wa mashtaka unadai kuwa mwanariadha huyo amemuua mpenzi wake huyo kwa makusudi baada ya ugonmvi wa kushambuliana kwa maneno , ambapo majirani walisikia.

Masipa alikuwa akifafanua upande wake wa mawazo kuhusiana na hukumu inayokuja katika kesi dhidi ya Pistorius, na kusema , hakukuwa na ushahidi wa kutosha , kutia nguvu maelezo ya mauaji ya kukusudia katika kifo cha Steenkamp.

Hapo mapema jaji huyo mwenye umri wa miaka 66, alitia shaka katika maelezo ya mashahidi ya kusikia ukelele ukipigwa na mwanamke, sehemu muhimu ya kesi ya upande wa mashataka.

Oscar Pistorius Mord Wohnhaus
Nyumba ya Oscar Pistorius yalipotokea mauajiPicha: picture-alliance/AP Images

Masipa amesema , "hakuna hata shahidi mmoja ambaye amesikia mshitakiwa akipiga kelele ama kupiga ukelele, wachilia mbali wakati akiwa na hasira ," akitambua uwezekano wa madai ya upande wa utetezi kwamba Pistorius ndie aliyekuwa akipiga ukelele kwa sauti ya juu baada ya kugundua kuwa amemuua kwa kumpiga risasi Steenkamp.

Katika wakati fulani , Masipa amesema: " Naendelea kueleza kwanini wengi wa mashahidi hawakutoa taarifa sahihi."

Pisorius ana hatia

Mmoja kati ya watu waliokuwapo mahakani na kuulizwa kuhusu maamuzi ya jaji huyo amesema Pistoriaus ana hatia.

"Ana hatia. Kitu kama hiki kimelishitua taifa la Afrika kusini. Bado tumo katika hali ya kushitushwa kwamba kitu kama hiki kimetokea."

Nao wanasheria na wasomi wa mambo ya sheria wameeleza kushitushwa kwao kutokana na kutupiliwa mbali kwa makosa ya mauaji dhidi ya Pistorius leo, huku wakosoaji wakisema Thokozile Masipa amekuwa na huruma sana.

Südafrika Sport Oscar Pistorius mit Freundlin Reeva Steenkamp
Pistorius na mpenzi wake Reeva SteenkampPicha: picture-alliance/AP

"Nimeshtushwa," amesema mwanasheria wa masuala ya uhalifu Martin Hood, baada ya Masipa kusema upande wa mashtaka haujaridhisha kesi yake ya mauaji ama mauaji ya kukusudia.

"Nafikiri atakosolewa vikali na mahakama na mfumo wa sheria ," amesema mwanasheria huyo mwenye makao yake mjini Johannesburg.

"Kwa ujumla ni kwamba amekosea." ameongeza mwanasheria huyo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape

Mhariri: Yusuf , Saumu