1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Njia rahisi ya kuendelea kuwa na Afya

1 Septemba 2008

Iwapo wasikilizaji wanataka kuwa na maisha yenye afya bora, hawana haja tena ya kusoma vitabu kwani kwa kusikiliza vipindi vya „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ inaweza kuwa hatua ya kwanza.

https://p.dw.com/p/DnNE
Picha: CORBIS

Malaria ni ugonjwa unaosababisha idadi kubwa ya vifo barani Afrika. Ugonjwa huo unasambazwa na mbu na unachukua maisha ya mtoto wa Kiafrika kila bada ya sekunde 30. Lakini kuna hatari nyingine kadhaa za kiafya. Chakula kinaweza kuoza haraka katika hali ya joto na maji ya kunywa ambayo hayakuchemshwa huenda yakasababisha maambukizi ya homa ya matumbo, taifod. Tatizo la unene pia linaongezeka katika nchi za kiafrika kama ilivyo katika nchi zilizoendelea kiviwanda.

Kukinga ni rahisi kuliko kutibu

Magonjwa mengi yanaweza kuzuiwa kwa urahisi, lakini watu wengi hawafahamu ni kwa vipi. Wakati mwingine, hifadhi sahihi ya chakula na kuangalia usafi ndio mambo yanayohitajika tu. Katika mchezo wa redio, „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ inakuwa karibu na wavulana watano ambao wameanza kuishi kwa kujitegemea. Wasikilizaji wake watajiunga nao wakati wakianza kugundua vitisho muhimu vya afya ndani na nje ya nyumba yao na njia rahisi za kuviepuka.

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa,Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.