1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Zealand ina mipango ya Kombe la Dunia

13 Aprili 2015

Ombi la New Zealand kuwa mwenyeji mwenza wa kombe la dunia mwaka 2026 ama 2030 linaweza kuwa ndoto ya mchana, lakini nchi hiyo inaendelea na mipango yake hiyo mikubwa.

https://p.dw.com/p/1F7Hc
Australia AFC Asia Cup Soccer (Iran vs. Qatar)
Picha: picture alliance/dpa/P. Miller

Mchezaji wa zamani wa mchezo wa kriketi Martin Snedden , ambaye ameongoza fainali zenye mafanikio za dunia katika mchezo wa rugby mwaka 2011 nchini humo , ameeleza uwezekano wa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia pamoja na Australia leo Jumatatu.

Azimio la kuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki mwaka 2024 lilipitishwa na baraza la halmashauri ya mji wa Paris leo, hatua inayosafisha njia kwa mji huo kuwasilisha ombi lake la kuwania nafasi hiyo katika kamati ya kimataifa ya olimpiki.

Rais Francois Hollande mwezi Novemba pia aliunga mkono juhudi za mji wa paris kuwa mwenyeji wa michezo hiyo ya Olimpiki.

Na katika tennis waziri mkuu wa India Narendra Modi ameongoza wimbi la sifa na pongezi zinazommiminikia Sania Mirza baada ya kuwa mchezaji wa kwanza wa tennis nchini humo kushikilia nafasi ya kwanza katika michezo ya wanawake kwa wachezaji wawili wawili.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf, Saumu