1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani mchezaji bora wa kandanda Afrika?

7 Novemba 2014

Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka barani Afrika Yaya Toure anaongoza orodha ya wachezaji watano wa Ligi Kuu ya England ambao ni miongoni mwa wachezaji 25 walioteuliwa na CAF kugombea tuzo ya mwaka huu

https://p.dw.com/p/1Dj7z
Bildergalerie Afrikanische Fußballspieler Yaya Toure
Picha: Getty Images/A. Livesey

Kiungo huyo wa Cote d'Ivoire yuko kwenye mkondo wa kutangazwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka wa nne mfululizo na anaonekana kuwa anayepigiwa upatu kwenye orodha hiyo baada ya kuisaidia Manchester City kushinda taji la Premier League msimu uliopita.

Wengine ni mwenzake katika timu ya taifa mshambuliaji Wilfried Bony wa Swansea City, kiungo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayechezea klabu ya Vrystal Palace Yannick Bolasie na kiungo wa Senegal Sadio Mane wa Southampton. Mshambuliaji wa Togo na klabu ya Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor, ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka wa 2008, pia yuko kwenye orodha hiyo.

Orodha kamili:

Ahmed Musa (Nigeria), Asamoah Gyan (Ghana), Dame N'doye (Senegal), Emmanuel Adebayor (Togo), Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon), Fakhreddine Ben Youssef (Tunisia), Ferdjani Sassi (Tunisia), Gervinho (Ivory Coast), Islam Slimani (Algeria), Kwadwo Asamoah (Ghana), Mehdi Benatia (Morocco), Mohamed El Neny (Egypt), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Raïs M'Bolhi (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Seydou Kieta (Mali), Sofiane Feghouli (Algeria), Stephane Mbia (Cameroon), Thulani Serero (South Africa), Vincent Aboubakar (Cameroon), Vincent Enyeama (Nigeria), Wilfried Bony (Ivory Coast), Yacine Brahimi (Algeria), Yannick Bolasie (DR Congo), Yaya Toure (Ivory Coast).

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu