1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msimu mpya wa Ligi Kuu ya England waanza

15 Agosti 2014

Kurejea kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Soka England wikendi hii kumewasisimua mashabiki wa ambao walikuwa wamekasarishwa na matokeo duni ya timu ya England katika dimba la Kombe la Dunia nchini Brazil

https://p.dw.com/p/1CvOz
Real Madrid vs. Manchester United 2.8.2014
Picha: Getty Images

Kutokana na utajiri wa ligi hiyo pamoja na umaarufu wake wa kimataifa, English Premier League inasalia kuwa mwamba wa soka la Uingereza. Lakini wakati namna ambavyo timu za Uingereza zilivyozembea katika jukwaa la Ulaya msimu uliopita, ushawishi wa Premier League unasalia kuwa chini ya kitisho kutoka kwa Uhispania.

Gareth Bale aliihama Tottenham na kujiunga na Real Madrid mwka jana, na msimu mpya unaanza na Luis Suarez akiwa Barcelona badala ya Liverpool. Liverpool walipata karibu dola milioni 130 kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Uruguay, na sasa haina mchezaji ambaye aliiejesha timu hiyo katika kundi la vigogo.

Manchester United inaonekana kuwa inayoweza kupanda juu zaidi kuliko Liverpool. Louis van Gaal amechukua nafasi ya David Moyes, ambaye alitwa amikoba ya Alex Ferguson kama meneja msimu uliopita lakini akawa na wakati mgumu uwanjani Old Trafford na hata kukosa kufuzu katika Champions League.

Fußball Liverpool vs. Chelsea
Chelsea na Liverpool ni miongoni mwa vigogo UingerezaPicha: Getty Images

Van Gaal tayari ana ujuzi aliopata katika vilabu vya Ajax, Barcelona na Bayern Munich. Pia aliiongoza Uholanzi kumaliza nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia Brazil. Arsenal iligonga vichwa vya habari kwa kumsajili Alexis SANCHEZ kutoka Barcelona na wengi watataria kuona namna timu ya Arsene Wenger itakavyofanya msimu huu. Mabingwa wa msimu uliopita Manchester City wanatarajia kutetea kombe hilo, na pia wamejiimarisha katika safu ya katikati na ulinzi.

Makocha wachache kama vile Jose Mourinho wamefanya biashara nzuri katika kipindi cha mapunziko. Ameitengenezea Chelsea dola milioni 115 kwa kuwauza David Luiz kwa Paris Saint Germain na mshambuliaji Romelu Lukaku kwa Everton. Na akatupia pesa alizopata kumnunua kiungo Cesc Fabregas kutoka Barcelona, mshambuliaji Diego Costa na beki Filipe Luis kutoka Atletico Madrid. Pia amemrejesha Didier Drogba mwenye umri wa miaka 36.

Leicester imerudi katika ligi baada ya kuwa nje kwa mwongo mmoja, Burnley inarejea baada ya miaka mitano, na Queens Park Rangers ikapanda daraja msimu huu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu