1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mourinho: Terry atachezea Chelsea msimu ujao

6 Machi 2015

Mkufunzi wa miamba ya ligi kuu ya Uingereza Premier League Chelsea ya mjini London Jose Mourinho amewahakikishia mashabiki wake kwamba mchezaji nguli John Terry atabakia msimu ujao

https://p.dw.com/p/1EmXi
Champions League Finale 2012
Picha: Reuters

Terry mlinzi wa kati mwenye umri wa miaka 34 ana mkataba wa mwaka mmoja utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu. Mourinho aliuambia mkutano na waandishi wa habari Jumatano kwamba anajuwa anachoambiwa na bodi ya kilabu na kile anachoambiwa na wachezaji wake na hakuna shaka yoyote Terry atapewa mkataba mpya kabla ya mwisho wa msimu huu na hilo anauhakika nalo. Mourinho akaongeza kwamba, utafika wakati kwa Chelsea kufikiria nania atajaza pengo litakaloachwa na Terry, lakini wakati huo bado haujafika.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Josephat Charo