1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Tabia Nchi na Wakimbizi Magazetini

22 Septemba 2014

Mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia nchi mjini New York,na Wimbi la wakimbizi ulimwenguni ni miongoni mwa mada zilizopewa kipaumbele na wahariri wa magazeti ya Ujerumani

https://p.dw.com/p/1DGkh
Maandamano ya mjini Berlin kuwazinduwa wanasiasa wachukue hatua kujikinga na mabadiliko ya tabia nchiPicha: Reuters/T. Peter

Tuanzie New York ambako mkutano wa kilele wa tabia nchi unatazamiwa kuanza kesho.Kabla ya viongozi wa kimataifa kukutana,jana walimwengu wameteremka majiani tangu New York mpaka katika sehemu nyengine za dunia kuwazinduwa walimwengu juu ya umuhimu wa kufikiwa makubaliano ya kuinusuru sayari yetu,mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi utakapoitishwa mwakani mjini Paris.Gazeti la Landeszeitung linakosoa ile hali kwamba kansela Angela Merkel hafungi safari kwenda New-York safari hii.Gazeti linsaandika:"Usemi wa kansela Angela Merkel "siasa ya ndani si muhimu"umempatia sifa nyingi katika majukwaa ya kimtaifa.Lakini kwamba "Mwanamke mwenye nguvu kabisa ulimwenguni,hatohudhuria kwa mara nyengine tena hadhara kuu ya Umoja wa mataifa na hata katika mkutano wa kilele wa tabia nchi, atawakilishwa na waziri wake wa mazingira bibi Hendricks,jambo hilo limewakera wengi mjini New-York.Kutokuwepo Merkel katika vikao hivyo kunadhoofisha juhudi za Ujerumani za kupigania kiti cha kudumu katika baraza la usalama.Pekee sifa inazojivunia Ujerumani kama mshika bendera wa juhudi za kuhifadhiwa tabia nchi ingekuwa sababu ya kutosha kwa kansela kuonekana katika mkutano kama huo wa kilele.Kwasababu bado kuna mataifa mengi tuu yanayobidi yafumbuliwe macho ili yatambue kwamba suala la tabia nchi limegeuka kuwa suala la kufa kupona kwa mamilioni ya watu.Na hilo halitowezekana bila ya kuwepo mikutanoni.

Idadi ya Wakimbizi ni kubwa kupita kiasi

Gazeti la Tagesspiegel linakumbusha sio Angela Merkel pekee atakaekosekana katika mkutano huo wa Tabia nchi.Hata rais wa India Narenda Modi na mwenzake wa China hawatohudhuria mkutano huo.Mtihani mwengine unaoitikisa dunia unahusiana na wimbi la wakimbizi ambalo gazeti la "Märkische Oderzeitung" linasema halijawahi kushuhudiwa tangu miaka 50 iliyopita.Gazeti linaendelea kuandika:"Zaidi ya watu milioni 51 na laki mbili,kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wameorodheshwa kama wakimbizi hadi mwisho wa mwaka 2013 na idadi hiyo imeonmgezeka bila ya shaka hivi sasa.Kutokana na hesabu hizo ni shida kuamini kwanini nchi za ulaya zinazozana.Kwa miezi sasa Italy imekuwa ikitoa wito wa mshikamano.Na hata kama Thomas de Maizière ameitika,lakini kwa masharti.Na mashartzi kama hayo hayawasaidii si wakimbizi na wala si serikali za miji wanakokutikana.Wanasiasa kutoka nchi zote za Umoja wa ulaya wanabidi wakubaliane mkakati jumla na kwa haraka.Kwasababu wanapoendelea kujipasua vichwa,maisha ya wengine yanaendelea kuangamia.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir(Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman