1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mfupi wa viongozi wa Umoja wa ulaya

19 Desemba 2014

Pengine ulikuwa mkutano mfupi kuliko yote iliyowahi kuitishwa hadi sasa na Umoja wa ulaya mjini Brussels,lakini safari hii hakujakuwa na mabishano na sera kuelekea Urusi zinajulikana;zimesalia vile vile

https://p.dw.com/p/1E7M5
Mkuu wa baraza la Ulaya,waziri mkuu wa Zamani wa Poland,Donald TuskPicha: AFP/Getty Images/T. Charlier

Maripota mjini Brussels wameduwaa:kwa mara ya kwanza kabisa mkutano wa viongozi wa taifa na serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa ulaya umemalizika siku moja kabla ya wakati.Kawaida viongozi hao wa mataifa 28 huendesha majadiliano makali yanayopelekea hata mikutano yao kuendelea hadi usiku wa manane na mara nyengine kurefushwa pia.

Safari hii,mwenyekiti mpya wa baraza la Umoja wa Ulaya,Donald Tusk alitamka baada ya karamu ya chakula cha usiku,iliyoaandaliwa baada ya saa tano za usiku "Tumemaliza."Kikao cha kesho ijumaa hakina haja ya kuitishwa.

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa kilele kusimamiwa na Donald Tusk.Alipokuwa waziri mkuu wa Poland alikwisha shiriki mara 47 katika mikutano kama hii ya kilele.Anatajikana kuwa mtu mwenye maarifa na aliyebobea.

Tusk alikuwa na mada mbili tu katika ajenda yake ya mazungumzo:Siasa ya siku za mbele ya Umoja wa Ulaya kuelekea Urusi na mpango wa uwekezaji wa Umoja wa Ulaya mpango uliolengwa kuinua shughuli za kiuchumi.Mada zote mbili,hazikuwa za mabishano makubwa.Zote nyengine zitajadiliwa mkutano mwengine wa kilele utakapoitishwa mwezi februari mwakani.

Hoja za rais wa Urusi hazina msingi

Katika sera zake kuhusu Urusi Umoja wa Ulaya unataka kuendelea na mkakati wa ncha mbili.Vikwazo vya kiuchumi viendelezwe wakati huo huo lakini kila la kufanywa lifanywe kusaka ufumbuzi wa kisiasa wa mzozo wa Mashariki ya Ukraine pamoja pia na kumezwa na Urusi raas ya Crimea ambayo ni sehemu ya ardhi ya Ukraine.

EU-Gipfel in Brüssel 18.12.2014 Merkel
Kansela Angela Merkel akijiandaa kuzungumza na waandishi habari mwishoni mwa mkutano wa kilele mjini BrusselsPicha: AFP/Getty Images/T. Charlier

Kiongozi mmoja tu,rais wa Lithuania Dalia Grybauskaite ndie anaeunga mkono msimamo mkali kuelekea Urusi.Hoja za rais Vladimir Putin kwamba Umoja wa Ulaya unabeba jukumu la mzozo wa umwagaji damu wa Ukraine imetajwa kuwa ni uwongo mtupu.Amezisuta pia hoja za Putin kwamba mgogoro wa kiuchumi na kuporomoka thamani sarafu ya Urusi Rubel ni matokeo ya vikwazo vya nchi za magharibi.

Mwakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya bibi Federica Mogherini ametahadharisha akisema "watu wasifurahikie mgogoro wa fedha wa Urusi kwasababu hautaiathiri pekee Urusi,bali pia Ukraine,Ulaya na sehemu iliyobakia ya dunia".

Kuhusu maombi ya Ukraine kusaidiwa haraka kifedha,viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekaa kimya.Wanasisitiza misaada ziada ya fedha itatolewa mageuzi ya kiuchumi na juhudi za kupambana na rushwa zitakapoanzishwa.

Kimsingi rais Petro Poroschenko alipendelea kuhudhuria kama shahidi mkutano huo wa kilele,lakini mwenyekiti wa baraza la Ulaya Donald Tusk,hakumwalika.

Ufafanuzi zaidi unahitajika kuhusu mpango wa uwekezaji

Ama kuhusu mpango wa vitega uchimi ulioshauriwa na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya,Jean Claude Juncker, viongozi wa Umoja huo wametoa ridhaa ya kimsingi tu.Wanataka kupata maelezo zaidi kuhusu mpango huo uliolengwa kuhimiza ukuaji wa kiuchumi .Mengi yanahitaji kufafanuliwa kwa mfano vitega uchumi hivyo vitagharimia miradi ya aina gani na nchi husika zitachangia vipi?Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya inapanga kuwasilisha ufafanuzi kuhusu miradi hiyo mwishoni mwa mwezi wa januari ili kupata ridhaa ya baraza la mawaziri na baadae bunge la Umoja wa Ulaya.

EU-Gipfel in Brüssel 18.12.2014 Juncker
Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya,waziri mkuu wa Zamani wa Luxemburg,Jean-Claude JunckerPicha: AFP/Getty Images/T. Charlier

Mwandishi:Riegert,Bernd/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Yusuf Saumu