1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanubi wanavyodumisha utamani ugenini

Geoffrey Mung'Ou5 Septemba 2014

Wanubi wameishi katika eneo la Kibera nchini Kenya kwa zaidi ya miaka 100. Historia yao katika eneo hilo ina mizizi yake katika vita kuu vya kwanza na vya pili vya Dunia. Ungana na Geoffrey Mung'Ou ujue mengi zaidi.

https://p.dw.com/p/1D7kZ
Kenia Wahlkampagne in Kibera Slum bei Nairobi
Eneo la Kibera lilianzishwa hasa kwa ajili ya makaazi ya WanubiPicha: Reuters

Wakati wa vita vya kwanza na pili vya dunia, watu wa jamii ya Nubi kutoka Sudan walijumuishwa katika jeshi la Mwingireza...kuendeleza mapigano dhidi ya jeshi la Ujerumani. Baada ya kuisha kwa vita hivyo Wanubi waliwekwa na Waingereza katika maeneo ya Kibera nchini Kenya na Bombo nchini Uganda, ambako wanaishi hadi sasa wakidumisha utamaduni wao.