1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Migogoro mikubwa yafunika mingine

29 Septemba 2014

Vita dhidi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu (IS) na kusambaa haraka kwa maradhi ya Ebola ni masuala makuu muhimu wakati huu. Yote yalijitokeza usoni zaidi mbele ya mkutano Baraza kuu la Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/1DMba
New York Rede Steinmeier UN-Vollversammlung 27.09.2014
Picha: Reuters/Eduardo Munoz

Lakini hakuna kilichoelezwa juu ya nafasi ya Umoja wa mataifa kama msimamizi kwani haukuwa Umoja huo bali ni rais Obama ndiye aliyetokeza kuwa mtu anayeshinikiza juu ya kuchukuliwa hatua za dharura dhidi ya Ebola na IS. Kwa hiyo Mkutano huo ulitawaliwa zaidi na Wamarekani katika hali isiyowahi kuonekana hapo kabla. Ufuatao ni uhariri ulioandikwa na Gero Schließ.

Uamuzi wa Obama wa kuushawishi Umoja wa mataifa juu ya mashambulizi ya angani nchini Syria katika mapambano dhidi ya kundi la Dola ya Kiislamu IS na kuingia katika awamu mpya, ni jambo lililothihirisha kuwa ni hatua mahiri. Hata kabla ya kuanza hotuba yake alifanikiwa kuishawishi hadhara kuu, juu ya haja ya kuutanua muungano dhidi ya IS. Mwishoni mwa juma zima la harakati katika Umoja wa mataifa hivi sasa kuna muungano ulio bega kwa bega zikijunga kuanzia Uingereza hadi nchi ndogo katika Ulaya kama Ubeligiji na Denmark. Jumuiya ya kimataifa imetambuwa hatari iliopo.

Mwandishi wa DW Gero Schliess.
Mwandishi wa DW Gero Schliess.Picha: DW/P.Henriksen

Baadhi miongoni mwa mataifa ya kihafidhina ya Kiarabu hivi wametokeza na msimamo ulio wazi. Hata Urusi nayo imekubaliana ana azimio la Obama dhidi ya wale wanaoitwa “ wapiganaji wa kigeni,” wanaopigana Iraq na Syria upande wa IS.

Kauli ya Ujerumani katika mazingira haya haikuwa rahisi kwa waziri wa kigeni Steinmeier, hasa kwa kuwa iliambatana na kile kisichotarajiwa kutajwa na Obama juu ya kushiriki kwa Ujerumani katika mashambulizi ya angani. Hata hivyo mwishowe alikuwa Steinmeier aliyeweza kucheza karata zake mwenyewe kwa mtazamo wa siasa za madola makuu. Kwa kutangaza mkutano wa kimataifa kuhusu wakimbizi mjini Berlin, ameweza kuchukuwa hatua kubwa na kuicheza karata ya Ujerumani. Kuonyesha uwezo katika utoaji misaada ya kibinaadamu.

Pia katika vita dhidi ya Ebola , uwezo huo unahitajika sana. Ingawa hapa Wamarekani kwa mara nyengine wako usoni wakiongoza, kutokana na Obama kutuma wanajeshi 3,000 na wahuduma wa afya katika nchi za kiafrika zilizoathiri8ka.

Kandoni mwa yote hayo kulizungumzwa pia mgogoro wa Ukraine mjini New York.

Alikuwa Stenmeiwer alipopanda jukwaani aliyeishutumu Urusi kwa kukiuka sheria. Waziri wa kigeni wa Urusi Lavrov alijibu akiushutumu upande wa Magharibi kwa mashambulizi ya angani dhidi ya mamlaka ya mipaka ya Syria, kwa kuwasaka wapiganaji wa IS na kuhujumu sheria ya kimataifa.

Habari njema hata hivyo, ni kuwa hatimae Urusi na nchi za magharibi zimeungana pamoja katika masuala makuu mawili ya mizozo. Mbali na vita dhidi ya IS pia kuna mgogoro wa mpango wa Nyuklia wa Iran. Msimamo katika mazungumzo safari hii ni mkali. Kwa jumla ,matokeo katika mjadala wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa mwaka huu yalikuwa na tija.

Ingawa Baraza Kuu hutawaliwa zaidi na siasa za wakati husika, suala la mazingira tabia lilipewa kipaumbele na Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia nchi.Lakini kuna mengine mazito kama uongezko la idadi ya watoto, ugawanyaji wa mali asili au upunguzaji silaha za nyuklia,-haya pia ni ya dharura

Mwandishi: Gero Schließ, DW/ Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Iddi Ssessanga