1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni : Nani anaihitaji bado OPEC ?

28 Novemba 2014

Kama ilivyotarajiwa mkutano wa shirika la mataifa yanayosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC,umemalizika jana kwa kukubaliana kutopunguza kiwango cha uzalishaji wa mafuta. Taasisi hiyo ina mamlaka gani kwa sasa.

https://p.dw.com/p/1DvfN
Rafael Ramirez beim OPEC Minister Treffen in Wien 27.11.2014
Waziri wa mafuta wa Venezuela Rafael Ramirez katika mkutano wa OPECPicha: Reuters/H. P. Bader

Anayeweza kujibu swali hilo kwa kweli hakuna . Ama kuna kundi la mataifa lenye ukiritimba wa bidhaa , ambalo linapanga bei kwa mfano kakao ama kahawa? Hakuna, bei zinapangwa na soko. Hata wale walanguzi wa kubahatisha katika masoko wanahusika.

Na iwapo kuna kundi la wenye ukiritimba, wadhamini wa ushindani watashindwa na hatimaye kuzuiwa. Kwa upande wa mafuta hilo halitokei. Kwanini basi?

Mafuta ni nyenzo muhimu

Kwa sababu mafuta ni nyenzo muhimu ya uchumi wa dunia. Kwa sababu ni nyezo pia ya kisiasa ya kutoa mbinyo. Na pia ni kwa sababu hatufahamu bado, kile tunachoweza kufanya na hazina hii kubwa ya mafuta ya ardhini.

Ni wazi kwamba watu wengi kwa sasa wanafurahia bei ya chini ya mafuta. Wanunuzi wa mafuta ya kutumia katika majumba yao kuleta joto , wasafirishaji bidhaa, wamiliki wa meli, na mashirika ya ndege.

Lakini kuna watu wengi tu ambao wana matatizo ya bei hiyo ya chini. Utawala wa Venezuela na Urusi kwa mfano.

Mataifa haya yanataka kupandishwa bei ya mafuta, kwa kuwa kwa hivi sasa wanapoteza mabilioni ya dola.

Deutsche Welle Henrik Böhme Chefredaktion GLOBAL Wirtschaft
Mkuu wa idara ya uchumi wa dunia katika DW Henrik BöhmePicha: DW

Yule anayetegemea sana mafuta , kwa wakati huu hana karata ya turufu.

Kuna hali kwa sasa ya nadharia ya kuporomoka kwa uchumi , kutokana na madeni wakati huu wa kuanguka kwa bei.

Saudi Arabia inataka washindani wake wanaochimba mafuta kwa mbinu za kisasa za Fraking, nchini Marekani kupiga magoti.

Wamarekani wanataka kuiadhibu Urusi kutokana na sera zake za kutaka kujipanua. Kwa pamoja katika kile kinachoitwa Dola la Kiislamu , ambalo linapata fedha zake kutokana na mauzo ya mafuta, wanataka chanzo hicho cha fedha kuzuiwa.

Na ipo hali halisi, ambayo ni uchumi dhaifu duniani. Matumizi ya mafuta kwa sasa yamepungua. Hapo kabla wakati ambapo dunia ilikuwa rahisi kuieleza shirika la OPEC lingeongeza uzalishaji, na kuiweka bei waitakayo.

Dunia haihitaji OPEC

Lakini dunia imekuwa kidogo yenye utata hivi sasa. Na OPEC imekuwa taasisi ya enzi za zamani. Marekani ambayo kwa sasa ni msafirishaji mkubwa wa mafuta haishiriki katika mkutano wao, na hata Urusi pia haimo. Kwa hiyo si jambo la kushangaza ,inaeleweka basi wakati Venezuela inatoa sauti kubwa wakati ikifikiria kuunda kundi la pili na Urusi , pembezoni mwa kundi hilo la OPEC.

Iwapo inawezekana, mtu anaweza kusema, lakini hakuna mtu anayetaka kununua mafuta kwa bei ya juu, wakati kuna muuzaji mwingine rahisi. Katika wakati huo OPEC huenda ikajifuta na haitakuwapo. Kitu gani kitakuwa kibaya? Wengine wana wasiwasi mkubwa.

Lakini mafuta rahisi kwa sasa ni tatizo kweli? Kutatua tatizo hilo dunia inahitaji kila fursa, lakini sio OPEC.

Mwandishi: Böhme, Henrik / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Daniel Gakuba.