1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malkia afungua rasmi michezo ya madola

24 Julai 2014

Malkia Elizabeth 11 amefungua rasmi michezo ya 20 ya jumuiya ya Madola jana katika sherehe kubwa mjini Glasgow ambapo mwanamuzi maarufu Rod Stewart aliwatumbuiza mashabiki waliohudhuria.

https://p.dw.com/p/1CiLh
Commonwealth Games / Glasgow
Gwaride la wanamichezo katika michezo ya Jumuiya ya Madola mjini GlasgowPicha: Reuters

Kiasi ya mashabiki 40,000 walijiunga katika sherehe hizo katika uwanja wa Celtic Park , ambako zaidi yaa wanariadha 4,000 kutoka mataifa 71 walifanya walipita mbele ya viongozi na maafisa wanaoandaa tamasha hilo.

Siku ya kwanza rasmi ya mashindano katika michezo hiyo ya jumuiya ya Madola mjini Glasgow imeanza leo Alhamis, ambapo medali 20 za dhahabu zinawaniwa katika matukio ikiwa ni pamoja na mbio za baiskeli , kuogelea, gymnastiki na matukio matatu kwa pamoja.

D-Day Feier 06.06.2014 Queen mit Prinz Charles und Valls
Malkia Elizabeth ameyafungua mashindano hayo rasmiPicha: Reuters

Mashujaa kuwania medali za dhahabu

Alistair Brownlee na Jonny Brownlee, wa Uingereza ambao walishinda medali ya dhahabu na shaba katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012, wanatarajiwa kushinda katika matukio hiyo matatu kwa wanaume, licha ya kuwa Richard Murray wa Afrika kusini anaonekana kuwa ni kitisho kwao.

Shujaa mwingine wa michezo ya Olimpiki iliyofanyika mjini London, Bradley Wiggins, anatarajiwa kuwania medali ya dhahabu katika mbio za baiskeli, tukio la pekee ambalo atashiriki , huku ikitarajiwa kutokea mpambano mkali baina ya mabingwa watetezi Australia na New Zealand, nchi ambazo zina washiriki wawili walioshinda katika mashindano ya mwaka 2014 katika vikosi vyao.

Leichtathletik WM Daegu 2011 Mo Farah
Mo Farah mkimbiaji wa UingerezaPicha: ap

Mo ajitoa

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Mo Farah amejitoa katika mbio mbili alizojiandikisha kukimbia katika michezo hiyo ya jumuiya ya Madola. Farah alijiandikisha kukimbia katika mbio za mita 5,000 na 10,000 katika michezo hiyo ya Glasgow kutokana na hofu juu ya hali yake kimchezo kufuatia kuwa mgonjwa, na kikosi cha timu ya Uingereza kimethibitisha uamuzi wake wa kujitoa kutoka mbio hizo licha ya kuwa anaonekana ameweza kurejea kiasi katika hali ya kawaida.

Katika mashindano ya Olimpiki mjini London mwaka 2012, Farah alishinda mbio za mita 5,000 na 10,000.

Mwandishi: Sekione Kitojo