1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makanisa yakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

2 Septemba 2014

Pamoja na Ujerumani kuwa katika hamasa ya kufanya mabadiliko ya matumizi ya nishati katika sera yake, kiwango cha hewa chafu, kumengezeka kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, kwa mara ya kwanza tangu muungano wake.

https://p.dw.com/p/1D5MH
Treffen der EU-Umweltminister
Mawaziri wa mazingira wa Umoja wa UlayaPicha: picture alliance/dpa

Hatua hii inatokana na uzalishaji wa umeme utokanao na makaa ya mawe. Jopo la wataalamu wa mabadiliko ya tabia nchi kutoka mataifa tofauti hivi Karibuni wamethibitisha kuwepo kwa uwezekano wa kudhibiti kiwango cha joto duniani chini ya nyuzi joto 2 katika kipimo cha Celcius. Lakini hata hivyo kumebainika kuwepo kwa kiwango kidogo cha kudhibiti hewa chafu katika kufanikisha lengo hilo na kuepusha kabisa na kasi ya mabadiliko ya tabia nchini.

Johannes Kapelle amekuwa akipinga vyombo vya muziki katika kanisa la Kipentekoste la Proschim tangu akiwa na umri wa miaka 14. miaka 78 sasa anajishughulisha na jamii katika uzalishaji wa nishati ya jua na amewalisisha watoto wake watatu pamoja na mke wake shughuli wanayoifanya shambani mwao Proschim, katika kijiji kidogo cha wakaazi 360,mjini Lusatia nchini Ujerumani.

Kutoweka kwa mandhari asilia

Hivi sasa analalamika kuwa shamba la kanisa, lenye msitu anaoupenda na kijiji chake chote kipo katika kitisho cha kuharibiwa kwa ajili ya kutoa nafasi ya upanuzi wa kampuni kubwa ya nishati ya Sweden-Vattenfall's lignite.

Umweltaktivisten protestieren am Montag, 31. Mai 2010, in Bonn
Wanaharakati wa mazingira wa mjini BonnPicha: AP

Kapele anaona hii inaleta ugumu katika mji wa Proschim hasa katika usambazaji wa nishati kwa jamii labda ikiwa itaweza kuhifadhiwa na kutengeneza gesi asilia.

Anaongeza kuwa labda inaweza kuchukua robo mwaka kuchoma makaa ya mawe hapa Proschim, na ardhi itaharibiwa milele. Nikimunukuu hapa anasema "hatuwezi kuwa na uwezo wa kuingia maeneo makubwa ardhini kwani kwa kufanya hivyo tutasababisha mmomonyoko wa udongo na hakutakuwa na uwezo wa kuotesha na kukuza chochote juu ya udongo, hakutakuwa na viazi, nyanya, hakutakuwa na chochote" alisema mwanamazingira huyo.

Kiasi cha kilometa 70 kaskazini mwa Proschim anapatikana mchungaji wa Kiprotestanti Mathias Berndt naye vile vile ana wasiwasi kuwa jamii yake inaweza kuathirika na kanisa lake limekuwepo kwa miaka 700 na lilinusurika katika vita vya karne ya 17, sasa linatakiwa kusaidia kutafuta njia kufunga mgodi wa lignite.

Mchungaji Atterwasch mwenye umri wa miaka 64, amekuwa Mchungaji tangu mwaka 1977 na anakataa jamii yake kutaka kuharibiwa. Anasema "Kama Wakristo, tuna wajibu wa kulima na kulinda viumbe wa Mungu; anasema katika Biblia tuko vizuri katika kulima lakini katika kuvilinda hatuko vizuri. Hivyo ndio maana nimekuwa nikijaribu kuzuia uharibifu wa asili tangu enzi ya Demokrasia nchini Ujerumani."

Kwa hivi sasa Berndt anajihusisha na maandalizi makubwa ya maandamano ya Agosti 23 yenye kuunganisha Ujerumani na baadhi ya vijiji vya Poland ambavyo vipo katika kitisho cha athari za mgofi wa makaa ya mawe. Vilevile amekuwa akichochea jitihada za kanisa lake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hii inatokana na Matokeo ya viongozi zaidi na imani yao ya pamoja ya uwekezaji. Mmoja wa watetezi wakubwa amekuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ambayo zamani alizawadiwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican Afrika Kusini Desmond Tutu, ambaye hivi karibuni aliitisha mgomo dhidi ya sekta ya nishati kama mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Uamuzi huo wa Tutu umeungwa mkono na Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na mabadiliko ya hali ya hewa, Christiana Figueres, ambaye ametoa wito kwa viongozi wa dini kuacha kuwekeza katika makampuni ya mafuta.

Mwandishi:Nyamiti Kayora
Mhariri:Josephat Charo