1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maisha Magumu – Wanawake na Wasichana

7 Januari 2010

Liberia inaongozwa na rais mwanamke. Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kutoka Kenya ni mwanamke. Wote wawili ni mfano kwa maelfu ya wasichana wa Kiafrika.

https://p.dw.com/p/DnLD
Picha: laif

Kuanzia katika umri mdogo, wasichana wengi watajifunza ni vipi wanapaswa kuwa wanawake katika Afrika ya leo: kuamka mapema, kupika na kufua nguo ni sehemu ya maisha ya kila siku. Nafasi yao kuweza kuyaacha maisha haya ni ndogo. Wengi wao wanawaona kaka zao wakienda shule wakati wao hawataweza kabisa kuingia darasani.

Wasichana wana haki pia

Kuwafanya wasichana watambue haki zao ni sehemu muhimu ya vipindi vya „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ ambavyo vimetayarishwa kwa ajili ya wasikilizaji wanaume na wanawake kwa pamoja. Kwa kusikiliza vipindi hivyo, wanaweza kupata kujua uwezo walionao wasichana na uwezo wanaoweza kuuendeleza.

Njia mpya

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ si kipindi halisi cha radio. Pia kitatoa mfululizo wa michezo ya redio juu ya wasichana na changamoto zao za kila siku. Taarifa zinafurahisha, zinatoa mwelekeo na baadhi ya nyakati zinakuwa za kuchekesha, lakini hazichoshi.

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinapatikana katika lugha sita, Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.