1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaraka kwa watu - Jamii na Afrika mpya

21 Mei 2010

Waafrika wengi zaidi wanajiunga na harakati za kutafuta maisha bora. Wanadai demokrasia, wanaandamana dhidi ya ufisadi na wanatilia nguvu zaidi maridhiano. Jamii yenye mwamko imejitokeza inayoweza kubadilisha hali.

https://p.dw.com/p/DnBz
Picha: achim Pohl/Das Fotoarchiv

Frederick Chiluba alifikiri ingekuwa safari rahisi. Katika mwaka 2002, alipendekeza kufuta kifungu katika katiba ambacho kinamkataza kugombea tena awamu ya tatu ya utawala kama rais wa Zambia. Lakini kwa mshangao mkubwa, upinzani wa jamii ulizuwia wabunge kutekeleza matakwa yake.

Enzi mpya

Katika nchi nyingi za Afrika, muda wa ufisadi na wanasiasa madikteta unakaribia mwisho. Licha ya matukio kadhaa ya kukatisha tamaa, watu wameanza kudai mengi kutoka kwa viongozi wao. Wanadai uwajibikaji na wanasiasa wademokrasi katika serikali zao, huku mashirika ya ndani na asasi zisizo za kiserikali zikisaidia kufanya sauti zao zisikike.

Madaraka kwa watu

Kuna sababu kadhaa zinazosababisha „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kulenga katika jukumu la jamii katika Afrika. Vipindi hivi haviishii katika jukumu la kisiasa, lakini pia vinawaelimisha wasikilizaji wake juu ya vipi jamii inaweza kusaidia katika kupunguza umasikini na kuimarisha maridhiano. Watakuwa katika safari na „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kutoka Liberia hadi Kenya ili kuangalia vipi watu wa kawaida wanapambana kupata Afrika mpya na yenye matumaini.