1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuuziba Mwanya wa Digital – Kompyuta na Mtandao

10 Mei 2012

Mwanya wa matumizi ya mtandao haujafutwa, lakini Afrika inakwenda kasi kufuta mwanya huo. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinatoa ushauri kwa kila mtu atayetaka kujiunga na dunia hii.

https://p.dw.com/p/DnKQ
Picha: CORBIS

Mtandao ni kituo kikubwa kabisa cha ufahamu na elimu. Shule na vyuo hivi sasa vinatoa mipango ya elimu ama hata digirii kamili kupitia mtandao. Ensaiklopidia katika mtandao zinatoa takwimu muhimu zikiwa na maelezo juu ya dunia na watu, zinapatikana katika vyumba vya maongezi, chatrooms, katika tabaka mbali mbali za tamaduni na mipaka ya nchi.

Taarifa kwa wale wanaotumia mtandao na wasiotumia

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinatoa vipindi vya aina mbali mbali vikiwa vinajishughulisha na masuala ya matumizi ya komyuta na internet. Vipindi hivi vinatoa fursa kwa watu wanaoanza pamoja na wale wataalamu katika dunia hii ya mambo ya electroniki kupanua ufahamu wao. Kwa kupitia kipindi cha „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ wasikilizaji wake wataweza kujifunza kila kitu wanachohitaji kufahamu juu ya taarifa za dunia, kuanzia kupata kompyuta sahihi ama internet cafe hadi kutumia mtandao katika kupata marafiki duniani kote.

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu:www.dw-world.de/lbe. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako" kinadhaminiwa na izara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.