1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutibu Ugonjwa wa Ebola

Kriesch, Adrian5 Desemba 2014

Mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola anaweza kupona endapo utagunduliwa na kutibiwa mapema, ingawa bado ugonjwa huu hauna dawa.

https://p.dw.com/p/1Dzf4
Ebola in Liberia (Behandlung im Krankenhaus)
Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Unapogunduliwa na ugonjwa wa Ebola sio mwisho wa maisha. Mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola anaweza kupona endapo utagunduliwa na kutibiwa mapema, ingawa bado ugonjwa huu hauna dawa. Hata hivyo, ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kupitia kutibu magonjwa ambayo ni dalili za Ebola, mfano kumeza dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuzuia kuzaana kwa viini mwilini na kupata lishe bora. Ni muhimu mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola kunywa maji mengi mara kwa mara, chai, na supu na ajiepushe kunywa pombe. Wagonjwa wa Ebola wanatibiwa katika vyumba maalum vilivyotengwa.

Ebola in Liberia (Behandlung im Krankenhaus)
Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Pengine unashangaa ni kwa nini madaktari na wauguzi huvalia mavazi ya kutisha yanayofunika mwili wote kuanzia kichwa hadi kwenye miguu, mfano wa mtu aliye kwenye mwezi, lakini unapaswa kufahamu kwamba wafanyakazi wote wa hospitali katika maeneo yanayokumbwa na Ugonjwa wa Ebola lazima wachukue tahadhari kwa kufunika kila sentimita ya mwili wao. Hii ndio njia pekee ambayo wataweza kuwahudumia wagonjwa wa Ebola.

Hata hivyo, katika muda wa miezi ya hivi karibuni, mazingira katika taasisi za matibabu na wodi za wagonjwa wa Ebola yameimarishwa sana hasa katika mataifa ya Afrika Magharibi. Yumkini asilimia 50 ya wanaoambukizwa virusi vya Ebola wanapona.

Na wakati mwengine, wagonjwa wanatibiwa kwa kutumia mchanganyiko wa dawa iliyotengenezwa kutokana na damu au chembechembe za kinga mwilini kutoka kwa Watu waliougua na kupona ugonjwa wa Ebola. Hata hivyo, tiba ya mchanganyiko wa aina hii haipatikani kwa urahisi, japo uchunguzi na juhudi za kutafuta dawa kwa Ugonjwa wa Ebola bado zinaendelea.