1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klose azitundika njumu zake

12 Agosti 2014

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Miroslav Klose, ambaye anashikilia rekodi ya kufunga mabao 16 katika michezo ya kombe la dunia ameamua kujiuzulu kuchezea timu ya taifa.

https://p.dw.com/p/1Csvg
Fußball WM Finale Argentinien Deutschland
Picha: AFP/Getty Images

Klose ni mchezaji wa pili wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyoshinda kombe la dunia mjini Rio kujiuzulu baada ya nahodha Philipp Lahm kutangaza kujiuzulu.

Wakati huo huo mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer atakuwa tayari kuchukua kazi ya unahodha wa timu ya taifa iwapo ataombwa kufanya hivyo akimrithi Philipp Lahm kama nahodha wa mabingwa wa dunia Ujerumani.

Manuel ambaye ametawazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka nchini Ujerumani mwaka huu amesema leo kuwa angemteua mchezaji wa kiungo iwapo angekuwa yeye ni kocha , lakini hatakataa wajibu huo iwapo ataombwa na kocha Joachim Loew.

Ujerumani inahitaji nahodha mpya baada ya nahodha wa Bayern Munich na timu ya taifa Philipp Lahm kutangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa siku tano baada ya Ujerumani kutawazwa mabingwa wa dunia baada ya kuishinda Argentina kwa bao 1-0 katika fainali Julai 13 mjini Rio de Janeiro.

Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Josephat Charo