1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipchoge ampiku Kipsang katika London marathon

27 Aprili 2015

Eliud Kipchoge ameongoza kikosi cha wakimbiaji kutoka Kenya jana kunyakua nafasi tatu za juu katika mbio za Marathon mjini London kwa kutumia saa mbili, dakika nne na sekunde 42

https://p.dw.com/p/1FFpB
London Marathon 2013
Picha: DW

Kipchoge bingwa wa dunia wa mita 5,000 alitumia maili ya mwili kuchomoka na kumuacha Wilson Kipsang, bingwa wa mwaka jana la London Marathon, wakati Dennis Kimetto anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo akitokea wa tatu.

Waandalizi wa mbio hizo walizipa jina la “mapambano ya mabingwa” ambapo Kimetto, aliyeweka muda bora ulimwenguni wa saa mbili, dakika mbili na sekunde saba mnamo mwezi Septemba katika mbio za Berlin marathon, alishiriki kwa mara ya kwanza jijini London wakati Mkenya Kipsang akitafuta taji lake la tatu baada ya kushinda mbio hizo mwaka wa 2012 na 2014.

Kimetto ambaye alivunja rekodi ya ulimwengu iliyowekwa na Kipsang mnamo mwaka wa 2013 kwa sekunde 26, ndiye mwanariadha wa kwanza duniani kukimbia chini ya saa mbili na dakika tatu.

Hata hivyo hakukuwa na uwezekano wa kuwekwa rekodi nyingine ya ulimwengu katika mbio hizo la London, kwa sababu barabara zilizopinda za zinafanya iwe vigumu kwa wanariadha ikilinganishwa na barabara zilizonyooka na pana jijini Berlin.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape / rtre
Mhariri: Yusuf , Saumu