1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yalaumiwa kutojibu haraka mashambulizi

24 Oktoba 2014

Wakala wa usimamizi wa jeshi la Polisi nchini Kenya umesema Vyombo vya usalama nchini humo vinahitaji kuboresha uratibu na miundo ya uongozi ili kuepuka kurudiwa kwa mashambulizi ya mwezi juni yaliyowaua watu 65:

https://p.dw.com/p/1Dawe
Demonstration in Nairobi Kenia 07.07.2014
Picha: picture-alliance/dpa

Ripoti iliyotolewa na mamlaka huru ya usimamizi wa polisi huru iliyotolewa siku ya iliotolewa Jumatatu imegusia juu ya malalamiko yaliosikika mwaka jana wakati wapiganaji wa Kiislamu walipolishambulia jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi. Pia imeashiria kwamba mapungufu bado hayajatatuliwa.

Watu waliokuwa na silaha waliwauwa watu kadhaa katika mji wa pwani wa Mpeketoni katika mwambao wa kaskazini, wakati wa shambulio la usiku mwezi Juni na kukivamia kijiji kimoja cha karibu usiku uliofuata. mashambulizi zaidi yalifanywa kwengineko mnamo mwezi Julai.

Wakazi katika eneo la pwani wamelalamika kwamba majeshi ya usalama yameshindwa kujibu mashambulizi hayo haraka na hayakutoa ulinzi baada ya matukio hayo. Maelfu ya watu walilikimbia eneo hilo.

Watu wakiangalia athari za shambulizi eneo la Mpeketoni
Watu wakiangalia athari za shambulizi eneo la MpeketoniPicha: REUTERS

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,Jibu la haraka lilishindikana kwa sababu ya amri zinazokinzana na ukosefu wa uongozi mkuu katika ngazi ya jimbo (kaunti) ambao unaweza kuratibu shughuli zote za polisi kitaifa katika mkoa huo.

Ikaongeza kwamba uchunguzi zaidi unapaswa kufanywa kuhusu swali , ni kwanini maafisa wa polisi wa Mpeketoni na wale wa utawala waliotarajiwa kuwa kwenye doria usiku wa tukio walikuwa hawakufika kazini wakati wa matukio hayo.

Maafisa wa zamani wa usalama pamoja na wa kibalozi, wanasema majeshi ya usalama nchini Kenya na idara za usalama wamekumbwa na uhasama unaohujumu mafunzo ya wataalamu kutoka Marekani, Uingereza na Israel pamoja na mataifa mengine

Ukosefu wa ushirikiano baina ya jeshi na polisi wakati wa shambulizi la Westgate lililozingirwa kwa siku nne Septemba mwaka jana pia ni sababu nyengine. watu wapatao 65 waliuwawa katika shambulizi hilo.

Watu wakikimbi kuokoa maisha yao wkati wa shambulizi la Westgate
Watu wakikimbia kuokoa maisha yao wakati wa shambulizi la WestgatePicha: Reuters

Ripoti kuhusu matukio ya Mpeketoni inasema mivutano ya kikabila, ardhi na dini miongoni mwa jamii za eneo hilo, imetumiwa kuwa sababu za wahusika kufanya shambulio lao.

Ripoti 37 miongoni mwa waliouwawa katika mashambulizi ya Mpeketoni ni kutokam kabila lam Kikuyu, anakotoka rais Uhuru Kenyatta ambao ni wahamiaji katika eneo hilo. wadadisi wanasema huenda mashambulizi hayo yamekuwa na lengo la kuchochea uhasama kati ya wakaazi wahamiaji na wale wanaojiona kuwa ndiyo wakaazi asilia wa pwani.

Mashambulizi hayo pamoja na kuwatia wasiwasi wakaazi, lakini yamewatia hofu watalii na kujizuwia kulitembelea eneo la Pwani, jambo ambalo limeathiri utalii, sekta muhimu kwa pato la fedha za Kigeni kwa Kenya.

Mwandishi: Nyamiti kayora/Reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman