Mjini Kisumu, Kenya katika kijiji cha Kogello kilomita kama 60 kutoka ziwa Viktoria, alikotoka Babake Obama, Hussein Obama,wakaazi wa eneo hilo wamekesha usiku kucha wakisubiri matokea ya uchaguzi huo.
Amina Abubakar amezungumza na Waandishi wetu John Marwa aliyeko Kisumu na Alfred Kiti akiwa Nairobi wakielezea shangwe, vifijo na nderemo pale Barack Obama alipotangazwa rasmi kuwa rais wa Marekani kwa kipindi cha pili.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Yusuf Saumu