1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Rais Kenyatta atangaza baraza la mawaziri

25 Aprili 2013

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelitangaza baraza lake la mawaziri, ambapo ameyapendekeza majina 16 yatakayofanyiwa uchunguzi na bunge kabla ya kuidhinishwa.

https://p.dw.com/p/18N8Q
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais Uhuru Kenyatta wa KenyaPicha: REUTERS

Hata hivyo jambo linalotarajiwa kuzusha mdahalo mkubwa ni kujumuishwa katika Baraza hilo majina ya wanasiasa wawili maarufu walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita. Majina hayo ni Najib Balala ambaye amependekezwa kuwa madini, wakati Charity Ngilu, akipendekezwa waziri mpya wa nyumba na makaazi. Muda mfupi uliopita nimezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya, Bobby Mkangi, ambaye kwanza alianza kwa kueleza sababu za Rais Kenyatta na naibu wake, William Ruto, kuchukua muda mrefu kulitangaza baraza hilo.

Mwandishi: Bruce Amani

Mhairri: Josephat Charo