Kimbunga kikubwa kilichoukumba mji wa Oklahoma nchini Marekani kimeuwa watu 91 wakiwemo watoto 20. Maafa makubwa yametokea katika kitongoji cha Moore, ambacho kimepitiwa na upepo unaosafiri kwa kasi ya Km 300 kwa saa.
Waziri mkuu mpya wa china Li Keqiang ameichagua India kuwa kituo cha kwanza cha ziara yake nchi za nje na kuahidi kurejesha hali ya kuaminiana kati ya Beijing na New-Delhi.
Wapiganaji 30 wa kundi la wanamgambo la Hezbollah wanaripotiwa kuuwawa katika mapigano yaliyotokea katika mji wa Qusayr nchini Syria huku wengine zaidi ya 70 wakijeruhiwa.
Rais wa Syria Bashar al Assad amesisitiza kuwa hatajiuzulu kabla ya mwisho wa kipindi chake madaraka mwaka 2014, wakati bomu lililotegwa katika gari liua watu watatu katika mji mkuu Damascus.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle Ijumaa (17.05.2013) ameyakinisha urafiki wa nchi yake kwa Israel katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa katika eneo hilo kutokana na mzozo wa Syria.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry anatarajiwa kusafiri kwenda katika mataifa ya mashariki ya kati na Afrika kuanzia Jumanne ijayo kwa ziara itakayomchukua hadi Mei 27.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anakutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais Barack Obama wa Marekani anafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki, Tayyip Erdogan, juu ya Syria.
Kimbunga Mahasen leo kimelipiga eneo la kusini mwa pwani ya Bangladesh kwa mvua kubwa na upepo mkali, hali iliosababisha zaidi ya watu milioni moja kuhamishwa kutoka eneo hilo.
Kiongozi wa chama cha upinzani Ujerumani SPD Steinbrueck (13.05.2013)amejaribu kuiweka sawa kampeni yake inayoyumba katika mkakati wa kupambana na kansela Angela Merkel katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mwanzoni alifahamika kama mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binaadamu, sasa Hassan Omar ni mwanasiasa akishikilia kiti cha useneta kutokea Mkoa wa Pwani nchini Kenya.
Kuwa shabiki wetu kwenye Facebook, tuchangiane mawazo.
Tembelea DW katika Twitter
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.