1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali nchini Misri na Homa ya uchaguzi Ujerumani

Oumilkher Hamidou21 Agosti 2013

Hali nchini Misri na suala kama wimbi la mageuzi katika nchi za kiarabu limekupwa,na suala la nani ataungana na nani baada ya uchaguzi mkuu Septemba 22 ijayo ndio mada zilizohanikiza magazetini.

https://p.dw.com/p/19S6t
Polisi wawaongoza wafuasi wa udugu wa kiislam toka msikiti wa Al Fath mjini CairoPicha: Reuters

Hali nchini Misri na suala kama wimbi la mageuzi katika nchi za kiarabu limekupwa, kashfa ya data za wagonjwa kupatiwa wabazazi wa kimarekani na suala la nani ataungana na nani baada ya uchaguzi mkuu Septemba 22 ijayo ndio mada zilizohanikiza magazetini hii leo. Tuanzie lakini Misri ambaako macho ya wahariri yamekodolewa kujua hatima ya kupimana nguvu serikali na wafuasi wa rais aliyepinduliwa Mohammad Mursi. Gazeti la "Rhein-Zeitung" la mjini Koblenz linaandika:

Mapinduzi yameijiongeza nchi hiyo ukiongoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wafuasi wa Udugu wa kiislam sio wa kulaumiwa. Hakuna anaeweza kuwakatalia wasilalamike dhidi ya kupinduliwa na kukamatwa rais wao aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia. Jumuia ya kimataifa inatakiwa sasa ionyeshe msimamo bayana. Kwa miongo kadhaa imekuwa ikiwaunga mkono watawala wa kiimla katika eneo hilo. Katika nchi za kiarabu,mpaka leo nchi za magharibi hazikusamehewa kwa hilo. Ndio kwanza nchi hizo zinajaribu kulirejea tena kosa hilo.

Wimbi la mageuzi limekupwa

Berliner Zeitung linahisi wimbi la mageuzi katika nchi za kiarabu linaanza kukupwa. Gazeti linaendelea kuandika:

Wafuasi wa Udugu wa kiislam wameuchukulia ushindi wa uchaguzi kuwa njia ya kunyakua madaraka na kutaka kuidhibiti Misri badala ya kuitawala. Na wanajeshi kwa kutwaa madaraka,wanafanya vivyo hivyo. Wanataka kwa mara nyengine tena Udugu wa kiislam upigwe marufuku. Mchunguzi mmoja anahisi: "Mapinduzi, ambayo kimsingi hayakutokea, yamekoma". Ni kweli, wimbi la mageuzi katika nchi za kiarabu limekupwa. Isitegemewe kuwa tawala nyengine katika eneo hilo zitaanguka.

Eti muungano wa vyama vikuu ndio bora?

Na hatimae homa ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani na kitandawili nani ataungana na nani kuunda serikali baada ya september 22? Gazeti la "Flensburger Tageblatt" linaandika kuhusu uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano wa vyama vikuu " na matukio yake......

Wapiga kura wanahisi muungano wa vyama vikuu,CDU/CSU na SPD,si mbaya hivyo. Na hakuna mwengine wanaoumezea mate,kama sio huo ambao wanahisi utaleta utulivu na kuaminika. Eti SPD wataridhia?Watakubali hawatashinda uchaguzi? Katu, kwa sababu wanahisi mjadala umezushwa mapema mno. Wanauangalia mjadala huu kama mbinu tu. Kwa sababu ikiwa wana SPD wakiamua kuteremka katika kampeni za uchaguzi na mada ya muungano wa vyama vikuu, watakaoathirika bila ya shaka ni FDP. Na kansela Merkel ana maoni sawa na hayo.Akiwaahidi mapema FDP, basi huenda akakabiliana na hali sawa na ile iliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2009, pale FDP waliposhurutisha kushiriki kwao serikalini.

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Khelef