1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za watoto barani Afrika - Vijana wenye uwezo

10 Mei 2012

Watoto wa Afrika mara nyingi wanapitia maisha magumu. Noa Bongo inajaribu kuangazia changamoto hizi na haki za kimsingi za watoto barani Afrika.

https://p.dw.com/p/MA9t
Maisha si matamu kama kipande cha keki kwa watoto wengi barani AfrikaPicha: LAI F

Huku watoto wengi wa Kizungu wanapokuwa wakicheza na Wanasesere, wenzao kutoka barani Afrika  wanalazimika kufanya kazi wakiwa wadogo sana. Katika mataifa mengi barani humu, watoto huenda shule wakati wa asubuhi na kisha kuwasaidia wazazi wao na kazi za shambani wakati wa alasiri. Isitoshe wengi wao hulazimika kuanza maisha ya kujitegemea wakiwa na umri mdogo sana kwa sababu wazazi wao wameshindwa kuwatunza.

Watoto barani humu wanapitia maisha magumu. Na wanakumbwa na tisho la  kufariki wakiwa na umri mdogo sana. Tisho la vifo miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ni kubwa zaidi barani Afrika kuliko mabara mengine. Baadhi yao wanaishi katika sehemu zinazokumbwa na mizozo na ukosefu wa usalama. Mbali na hayo si rahisi kupata elimu bora ikilinganishwa na wenzao kutoka mabara ya Asia, Marekani na  Ulaya.

Noa Bongo inaangazia  hadithi ya kuhuzunisha kuhusu masaibu ya  Watoto barani Afrika. Yote haya ni kutokana na juhudi zao wenyewe, na pia za watu  wanaotetea haki za watoto katika juhudi za kubadilisha maisha yao. Pia tunaangazia ufanisi uliopatikana, kwa mfano kuanzishwa kwa bunge  la watoto linalotetea haki za watoto nchini Nigeria.  

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika  lugha sita: Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharik. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni nchini Ujerumani.