1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yashinikizwa kuhusu maandalizi ya Kombe la Dunia 2022

19 Mei 2015

Kundi la kuweka mbinyo linalojulikana kama FIFA Mpya sasa na chama cha kimataifa cha wafanyakazi, leo vimewaeleza wafadhili wa shirikisho la kandanda duniani FIFA kuipa changamoto shirikisho hilo

https://p.dw.com/p/1FRow
Arbeiter Doha
Picha: picture-alliance/dpa

Ili liweze kushughulikia kwa makini visa vya ukiukaji wa haki za binadamu katika ujenzi wa viwanja fitakavyofanyika fainali ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

New FIFA Now linafanyakazi pamoja na shirikisho la vyama vya wafanyakazi duniani ITUC pamoja na baraza la umoja wa vyama vya kibiashara likiungwa mkono na Fair Paly Qatar kuyataka mashirika yanayolifadhili shirikisho hilo la kandanda kuhusu haki za wafanyakazi walioajiriwa katika ujenzi wa viwanja vya kombe la dunia.

Wakati huo huo rais wa shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA Michel Platini amesema sheria zinazozuwia matumizi ya fedha za uhamisho wa wachezaji na mishahara huenda zikalegezwa mwezi ujao. Shirikisho hilo kamati tendaji itakutana Juni 29-30 mjini Prague ambapo baadhi ya sheria zitalegezwa. Hata hivyo UEFA na chama cha vilabu barani Ulaya vimekataa kusema lolote juu ya taarifa za mapendekezo ya mabadiliko hayo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe 7 dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga