1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Esther Zawadi Panga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

23 Mei 2013

Esther Zawadi Panga ana umri wa miaka 28. Anafanya kazi kama daktari wa kupiga sindano za ganzi mjini Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Anahisi Umoja wa Afrika haulingani na wakati.

https://p.dw.com/p/18c3u
Fotograf ist John Kanyunyu, Korrespondent der Französischen Redaktion. Das Foto zeigt die Anästhesistin Esther Zawadi Panga, das Bild wurde in Goma, Denmokratische Republik Kongo, aufgenommen. Zulieferer: Friederike Müller
50 Jahre Afrikanische UnionPicha: John Kanyunyu

Umoja wa Afrika ni jumuia kongwe. Kwetu sisi Waafrika, hauna maana yoyote. Unahitaji kuangalia nchi kama Mali tu, utaona badala ya Umoja wa Afrika, Ufaransa ndio iliyoingilia kati. Nchini mwetu, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa zaidi ya miaka 10 tunaishi katika vita. Umoja wa Afrika ungebidi ulete wanajeshi wake huku na sio Umoja wa Mataifa. Ninataraji Umoja wa Afrika utafanyiwa marekebisho. Kwa sababu hauchangii kuyapatia ufumbuzi matatizo ya bara la Afrika.