1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ebola yawafukuzisha kazi mawaziri Liberia

Admin.WagnerD27 Agosti 2014

Rais wa Liberia amewafukuza kazi mawaziri na maafisa wengine waandamizi ambao wameshindwa kufanikisha jitihada za taifa hilo la Afrika Magharibi katika kukabiliana na maradhi ya Ebola

https://p.dw.com/p/1D1mU
Ebola West Point Liberia
Eneo lililobainika kuwa na Ebola LiberiaPicha: Reuters

Rais Johnson Ellen Sirleaf aliwaambia waziri wa walioko nje kurejea nyumbani kama sehemu ya dharura aliyoitangaza tarehe 6 mwezi huu, akionya kwamba hatua kubwa zinapaswa kuchukuliwa katika kukabiliana na janga hilo.

Sirleaf vilevile alitoa maelekezo kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya wizara, wakubwa na wadogo, wakurugenzi na manaibu wao ambao hawakuteleza hatua hiyo kuondoka mara moja katika nyadhfa zao. Hata hivyo taarifa kutoka katika ofisi ya rais huyo haikuweza kutaja idadi ya maafisa walioathiriwa na amri hiyo.

Lakini hata hivyo taarifa kutoka serikali zinasema adhabu hiyo imewagusa naibu mawaziri na maafisa waandamizi na sio mawaziri kamili.

Jitihada za WHO kkubaliana na ebola

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameahidi kuongeza jitihada zaidi dhidi ya virus vinavyosababisha ugonjwa huo hatari, ambao umeathiri zaidi ya watu 2,600 na kusababisha vifo vya watu 1,427 tangu kuibuka kwake mwanzoni mwa mwaka huu.

Liberia Ebola 24.08.2014
Zoezi la kupima dalili za Ebola nchini LiberiaPicha: picture alliance/AP Photo

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO Jumatatu hii lilisema zaidi ya wafanyakazi 120 wa sekta ya afya katika maeneo tofauti ya Afrika Magharibi wamepoteza maisha katika kipindi cha mripuko usio wa kawaida wa ugonjwa huo na wengine zaidi ya 240 wameathiriwa.

Nchini Siera Leone kwa mfano WHO imeondoa wahudumu wake wa afya kwa muda katika kituo cha Kailahun baada ya mmoja kati ya wafanyakazi hao kuathirika na kwamba uchunguzi unaendelea zaidi lengo ikiwa kudhibiti maradhi hayo yasienee zaidi kabla ya kuirejesha timu hiyo ya watoa huduma katika eneo hilo.

Taarifa ya mwakilishi mkazi wa WHO nchini Sierra Leone,Dokta Daniel Kertesz, ilisema "walipaswa kufanya hivyo kwa sababu timu hiyo ilikuwa katika hali ya kiwewe baada ya kubainika kuwepo kwa maambukizi ya Ebola miongoni mwao".

Mashaka ya baa la njaa Afrika Magharibi

Katika hatua nyingine Benki ya Maendeleo ya Afrika imesema mripuko wa Ebola utashusha kiwango cha ukuaji wa uchumi katika mataifa matatu yaliyoathriwa vibaya zaidi, sambamba na Ivory Coast, kwa kati ya asilimia 1 na 1.5.

Rais wa Benki hiyo Donald Kaberuka alisema kama watu hawataanza kujishughulisha katika kilimo kutakuwa na tatizo la upatikanaji wa chakula. Kwa hiyo hilo litakuwa tatizo la moja kwa moja kwa wakulika katika ukanda huo.

Kwengineko mfanyakazi mwingine wa WHO ambae amepata maambukizi ya Ebola nchini Sierra Leone anatarajiwa kuletwa hapa Ujerumani katika mji wa Hamburg kwa ajili ya matibabu. Msemaji wa Seneti ya Afya mjini Hamburg amesema afisa huyo ana asili ya Senegal.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga