Visiwani Zanzibar raia mmoja wa Tanzania Suleiman Abdala Salim alikamatwa nchini Somalia na kuzuiliwa nchini Afghanistan kwa madai ya kuhusika na ugaidi.
Mwanamume huyo aliyekuwa mvuvi alikuwa akifanya biashara yake katika maeneo ya Somalia na Visiwani humo alipokamatwa.Alizuiliwa kwa kipindi cha miaka minne nchini Afghanistan chini ya ulinzi mkali na kuteswa kwenye jela ya kituo cha jeshi la Marekani cha Baghram.Baada ya hapo aliruhusiwa kurudi nyumbani na kusaidiwa na Shirika la Msaada la msalaba mwekundu Redcross.
Mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said alikutana na Suleiman Abdala Salim punde alipowasili visiwani.Anaanza na kueleza jinsi alivyokamatwa nchini Somalia