Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita-ICC, Luis Moreno-Ocampo, amewasili nchini Kenya.
Luis Moreno Ocampo yupo nchini Kenya
Baadaye leo atafanya mazungumzo na viongozi wa Kenya, juu ya hatua za kushtakiwa watuhumiwa wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Grace Kabogo amezungumza na Hassan Omar Hassan, Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binaadamu nchini Kenya na nilianza kumuuliza nini matarajio ya Wakenya kutokana na ziara hii ya Ocampo.
Mahojiano: Grace Patricia Kabogo/Hassan Omar Hassan
Mhariri: M.Abdul-Rahman