1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kibaki azuia mswada wa wabunge kujipatia marupurupu

10 Oktoba 2012

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ameuzuia mswada wa sheria ambao ungewawezesha wabunge kujipatia marupurupu kiasi cha dola 110,000 watakapomaliza mihula yao ya kazi bungeni mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.

https://p.dw.com/p/16NPg
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: dapd

Uamuzi wa jana wa Kibaki ulifuatia kilio cha wananchi wakati nchi hiyo ikiwa imepandisha kodi zake kuziba pengo katika mahitaji yake ya fedha huku ikikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Josephat Charo amekusanya maoni ya baadhi ya wakenya kuhusu uamuzi wa rais Kibaki.

(Kusikiliza maoni hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman