1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Tanesco kupiga mnada nyumba za wanaodaiwa deni la umeme

20 Agosti 2012

Meneja wa uhusiano wa shirika la Umeme nchini Tanzania, Badra Masoud, amewaonya wezi wa umeme nchini kwamba shirika lake liko mbioni kuwakamata wezi wote na kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na shirika hilo.

https://p.dw.com/p/15stI
Shirika la Tanesco kufanya zoezi la kukagua wasiolipa umeme
Shirika la Tanesco kufanya zoezi la kukagua wasiolipa umemePicha: Fotolia/ Markus Schmid

Meneja wa uhusiano wa shirika la Umeme nchini Tanzania, Tanesco, Badra Masoud, amewaonya wezi wa umeme nchini humo kwamba shirika lake liko mbioni kuwakamata wezi wote na kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na shirika hilo.

Badra amesema baada ya wiki mbili shirika lake litaanza kupiga mnada nyumba za watu pamoja na  za kampuni kubwa kubwa nchini humo ambazo zinazodaiwa na TANESCO. Hata hivyo, Badra Masoud amesema shirika hilo pia litaanza mikakati ya kupambana na wafanyakazi walaji rushwa ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao. 

Awali Amina Abubakar alizungumza na Badra Masoud na mwanzo alitaka kujua zaidi juu ya mikakati hiyo ya Tanesco katika kuwakamata wezi wa umeme....

Insert

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri Othman Miraji