Huenda visa vya kigaidi vikaongezeka duniani kufuatia kundi la Al Qaeda kutangaza wazi kwamba kundi la waasi nchini Somalia Al shabaab limejiunga rasmi na wanamgambo hao wa kigaidi.
Wanamgambo wa Al Shabab
Msemaji wa kundi la Al Qaeda Ayman al Zawahri jana alitoa video ya dakika 15 inayoeleza maelezo hayo kwa kina na kusema kwamba sasa wataimarisha mapambano yao dhidi ya maadui zao.
Kwa kuchambua zaidi swala hili nimezungumza na Emmanuel Kisyangani mtafiti mkuu wa maswala ya Somalia katika taasisi ya kimataifa ya usalama ilio na makao yake mjini Nairobi.
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Othman Miraji