Vikosi vya Syria hii leo (08.02.2012) vimeyashambulia maeneo ya mkoa wa Homs kwa siku ya tano mfululizo, na kuwauwa karibu watu 47. Eneo hilo ni kitovu cha maandamano ya kuupinga utawala wa Assad.
Ugiriki imesema bado inakabiliwa na changamoto kubwa kushawishi Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha Ulimwenguni, IMF, kuipatia mkopo mwingine wa kunusuru uchumi wake na kitisho cha kufilisika.
Matumaini kwa mwaka 2012,mbinu za Iran ,miaka 10 tangu sarafu ya pamoja ya Euro ilipoanzishwa na hali nchini Iraq ni miongoni mwa mada zilichambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.
Shirika la kutoa msaada la madaktari wasio na mipaka - Medicins Sans Frontieres (MSF)-litawahamisha baadhi ya wafanyakazi wake kutoka Somalia baada ya wafanyakazi wake wawili kuuwawa jana mjini Mogadishu.
Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hivi leo (29.12.2011) wanazungumzia juu ya Korea ya Kaskazini baada ya kifo cha Kim Jong Ill na pia juu ya Poland kujiunga na Umoja wa sarafu ya Euro.
Maelfu ya watu nchini Syria wamemiminika katika barabara za nchi hiyo katika maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miezi kadhaa, wakiitisha kuvunjwa kwa utawala wa sasa wa rais Bashar al Assad.
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ameihakikishia jamii ya Kikristo nchini mwake kwamba serikali itachukuwa hatua kali kabisa dhidi ya makundi yote yanayofanya mashambulizi ya kigaidi kwa jina la imani za kidini.
Kocha Joachim Loew anahisi hamu ya kushinda taji akiwa na timu yake huku Ujerumani ikijitosa katika kivumbi cha ubingwa wa ulaya ikiwa na matumaini makubwa ya kunyanyua kombe lao la kwanza kuu katika miaka 16.
Katika uandishi habari, mtu anapomg'ata mbwa ndiyo inakuwa habari nzito, lakini mbwa anapomg'ata mtu ni jambo la kawaida.Kwa mtazamo huu, waandishi habari wanapolumbana na wenye madaraka waandishi wanajikuta mashakani.
Wananchi katika majimbo tisa ya Misri wanapiga kura katika duru ya tatu ya uchaguzi wa wabunge. Majimbo hayo ni ngome ya vyama vya Kiislamu, ambavyo vimepata ushindi katika duru za awali.