Zambia imeshinda taji lao la kwanza la mataifa ya bara la Afrika mjini Libreville, mji ambao miaka 19 iliyopita umekuwa eneo la mkasa mbaya zaidi kuwahi kuikumba soka ya nchi hiyo.
Timu ya taifa ya Zambia , Chipolopolo imeandika historia jana mjini Libreville ilipoweza kutoroka na taji la ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza , baada ya kujaribu mara tatu kufika fainali.
'Chipolopolo' wa Zambia na 'The Elephants ' wa Cote d'ivoire ndio watakaokutana katika fainali ya kombe la mataifa ya bara la Afrika baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali.
Mashindano ya kandanda ya Kombe la Mataifa ya Afrika sasa yameingia nusu fainali baada ya michuano ya robo fainali ya mwisho wa wiki, huku waandalizi wa mashindao hayo, Gabon na Guinea ya Ikweta, zikiyaaga.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.de.
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.