1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

David Ginola atangaza kuwania urais wa FIFA

16 Januari 2015

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola amezindua ombi ambalo kiasi kikubwa linaonekana tayari kutokuwa na mafanikio yoyote la kuwania urais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni – FIFA.

https://p.dw.com/p/1ELo5
David Ginola Bewerber FIFA Präsidialamt
Picha: REUTERS/N. Hall

Ginola ameanzisha kampeni ya “bingwa wa mashabiki” chini ya kauli mbiu ya “kuiamsha tena kandanda”.

Ginola mwenye umri wa miaka 48, ambaye ana hadi Januari 29 kudhihirisha kuwa anaungwa mkono na mashirikisho matano ya kandanda kabla ya ombi lake linaweza kukubaliwa rasmi na FIFA, anatafuta uungwaji mkono wa mashabiki kote ulimwenguni kumsaidia kuwa mmoja wa wagombea na kisha kuanzisha kampeni yake ya uchaguzi yenye mafanikio.

Wakati akizundua kampeni ya “Team Ginola”, mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle United, Tottenham Hotspur na Everton, amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini ana sifa na tajriba inayohitajika ili kuwa mgombea imara, mgombea wa mashabiki wa kandanda na wapenzi wa mchezo huo kutoka pembe zote nne za ulimwengu. Blatter amekuwa Rais wa Fifa tangu mwaka 1998 anawania muhula wa tano sasa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu